Niko tayari kufanya collabo na Diamond au Ali Kiba - Mr Blue

Hivi sasa katika mitandao ya kijamii wasanii wanaobattle kwenye vichwa vya habari na kutengeneza ‘kick ya story’ ni Diamond na Ali Kiba.

Kwa hiyo ni kawaida mstari mmoja unaowahuwahusu kutengeneza story ya aya tano kwa kuwa wanapendwa sana na mashabiki.  
Rapper wa Micharazo na BOB, Mr Blue amekutana na swali hilo wakati anaongea na mtandao wa Bongo5 ambao ulitaka kupata mtazamo wake ni yupi kati ya wakali hao angependa kushirikiana nae kwenye wimbo wake hivi karibuni.
“Unajua mimi wale wote washikaji zangu na wala sina tatizo nao, kwa hiyo niko tayari kufanya kazi na yeyote yule ambaye atakuwa tayari. Si unajua hii kazi na kazi mkishirikiana pamoja ndio inakuwa nzuri zaidi.” Amesema.
Mr Blue anatarajia kuachia video muda kwa wowote zilizoongozwa na Adam Juma, Pesa na Mapenzi.

Post a Comment

Previous Post Next Post