Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Mwenge –Tegeta
yenye urefu wa kilometa 12.9 katika eneo la Lugalo, jijini Dar es
salaam.
Taarifa iliyotolewa leo jijini
Dar es salaa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Muhandisi Musa Iyombe
imeeleza kuwa sherehe za ufunguzi wa barabara hiyo zitafanyika tarehe 1,
Oktoba ,2014 katika eneo la Lugalo njia panda ya Kawe kuanzia saa nne
asubuhi.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa
kukamilika kwa upanuzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 12.9 ni
sehemu ya mkakati wa serikali wa kupunguza msongamano wa magari katika
jiji la Dar es salaam.
Post a Comment