
Afisa
Habari, Elimu na Mawasiliano wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa
Vitendo Tanzania (Law School) Bi. Scholastica Njozi akiwaeleza jambo
waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa ziara iliyofanywa kwenye
Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Habari wa Wizara ya
Katiba na Sheria Bw. Omega Ngole.
Frank Mvungi-Maelezo
Serikali yatumia zaidi ya Bilioni 16 kujenga Taasisi ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo (the law school of Tanzania).
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Msemaji wa Wizara ya Katiba na
Sheria Bw. Omega Ngole wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika
taasisi hiyo iliyolenga kuona hatua iliyofikiwa tangu kuanza kwa ujenzi
wake mwaka 2010.
“Baada
ya kukamilika kwa ujenzi huu mwaka 2013 uendeshaji wa mafunzo ulihama
kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam na kuanza kutumika kwa majengo haya
ya kisasa yaliyojengwa na Serikali kupitia Wizara ya Katiba na sheria”
Akifafanua
Ngole amesema ujenzi huo umehusisha ujenzi wa Mahakama ya mafunzo,
(Teaching Court) vyumba vya madarasa (leacture theartres),Maktaba ya
Kisasa (Library) Jengo la Utawala ( Admistration block) Mgahawa na
nyumba za watumishi.

Afisa
Habari wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Omega Ngole akiwaleza
waandishi wa habari lengo la uanzishwaji wa Taasisi ya Mafunzo ya
Vitendo kwa wahitimu wa shahada ya kwanza ya sheria ikiwa ni kuwaongezea
ujuzi na stadi za kazi kwa ajili ya kutoa huduma bora na yenye tija ka
wananchi, wakati wa ziara iliyofanywa kwenye Taasisi hiyo Jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Taasisi ya
Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Bi. Scholastica
Njozi.
Pia
Ngole alitoa wito kwa wanasheria wote wanaohitimu katika Taasisi hiyo
kuwa tayari kutoa huduma popote pale nchini Tanzania kwa kuwa Serikali
imetumia fedha nyingi kuanzisha Taasisi hiyo ili iwanufaishe wananchi
wote.
Kwa
upande wake Mkuu wa Kitengo cha mitihani bw. Ipyana Mwaikambo alisema
Taasisi hiyo imeshadahili wanafunzi zaidi ya 4000 toka kuanzishwa kwake
mwaka 2008 hadi sasa.
Naye
Mmoja wa wanafunzi wa Taasisi hiyo Bw. Edwin Rweykaza amesema Taasisi
hiyo inatoa msisitizo katika mafunzo ya vitendo na kuwajengea uwezo wa
kutimiza majukumu yao mara baada ya kuhitimu.
Kuhusu maadili Rweykaza alibainisha kuwa ni swala linalopewa kipaumbele kwa wanafunzi wote wanaojiunga na Taasisi hiyo.
Serikali
imetimiza ndoto ya miaka mingi ya kujenga majengo ya kisasa ya Taasisi
ya Mafunzo ya uanasheria kwa vitendo Tanzania (The law school of
Tanzania) inayotoa mafunzo kwa vitendo kwa wahitimu wa shahada ya kwanza
ya sheria wanaotarajia kufanya kazi kama mawakili kwa lengo la kuongeza
stadi na ujuzi wa wanasheria hao katika kuwahudumia wananchi.

Mwanafunzi
wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School)
Bw. Edwin Rwekaza akiwaleza waaandishi wa habari kuhusu msisitizo
unaotolewa na Taasisi hiyo katika mafunzo kwa vitendo ili kuwaongezea
ujuzi katika utekelazaji wa majukumu pindi watakapo hitimu, wakati wa
ziara iliyofanywa kwenye Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria
kwa Vitendo Tanzania (Law School) Bi. Scholastica Njozi.

Mhadhiri
wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School)
Emil Lukiko akiwaeleza jambo waandishi wa habari (Hawapo pichani) ,
wakati wa ziara iliyofanywa kwenye Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Taasisi ya Mafunzo ya
Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Bi. Scholastica Njozi.

Mkuu
wa Kitengo cha Mitihani wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo
Tanzania (Law School) Ipyana Mwaikambo akiwaeleza waandishi wa habari
(Hawapo pichani), Kuhusu idadi ya wanafunzi waliodahiliwa toka Taasisi
hiyo imeanzishwa ambapo alisema zaidi ya wanafunzi 4000 wameshadahiliwa
mpaka sasa, wakati wa ziara iliyofanywa kwenye Taasisi hiyo Jijini Dar
es Salaam. Kulia ni Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Taasisi ya
Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) Bi. Scholastica
Njozi.


Jengo
la Kufundishia(Teaching Block) katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria
kwa Vitendo Tanzania (Law School) lenye vyumba 2 vya mihadhara(lecture
rooms) vyenye uwezo wa kuingiza wanafunzi 460 kila chumba, vyumba 72 vya
semina.

Jengo
la Mahakama ya kujifunzia (Teaching Court) lililopo katika Taasisi ya
Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (Law School) litalofungwa
Video Link ili wanafunzi waweze kujionea moja kwa moja namna kesi
zinavyoendeshwa.

Muonekano wa ndani wa chumba mihadhara(lecture rooms).

Muonekano
wa ndani wa Chumba cha Mahakama katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria
kwa Vitendo Tanzania (Law School).(Picha na Hassan Silayo- MAELEZO).
Post a Comment