KAMISHNA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Suleiman Kova leo, ametoa taarifa maalum ya Jeshi la Polisi kuhusiana
na mafanikio katika utendaji wao wa kazi.
Kova ametoa taarifa ya matukio yaliyojitokeza katika kipindi cha
wiki mbili ikiwemo operesheni maalum ya kuzuia kupambana na matishio ya
uhalifu jijini Dar es Salaam, mtandao wa uhalifu wanaotumia teknolojia
ya mawasiliano (IT).
Kukamatwa kwa majambazi sugu wawili pamoja na SMG, kukamatwa kwa
tiketi bandia 424 za mechi ya ngao ya hisani kati ya Yanga na Azam
pamoja na Kupatikana kwa silaha aina ya Pistol na risasi 6.
(Habari/Picha na Gabriel Ng’osha/GPL)
Post a Comment