Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Zaka na Sadaka Zanzibar (JUZASA) Shekh Said Suleiman
Masoud Mwenyekoti Jeusi akitoa nasaha zake kwa Wanachama na Waalikwa
katika Mkutano wa Jumuiya hiyo uliofanyika Ukumbi wa Shamtimba
Kiembesamaki Zanzibar.
Katibu
wa Jumuiya ya Zaka na Sadaka JUZASA Omar Abubakar akionesha Picha ya
Kibanda kilichokuwa kinakaliwa na Mama mmoja maskini ambapo kupitia Zaka
walizokusanya waliweza kumjengea nyumba Mama huyo aliyekuwa akiishi na
Mtoto wake Yatima Kisiwani Unguja.Kulia ni Mwenyekiti wa JUZASA Skh.
Said Suleiman Masoud.
Kukosekana
kwa Utaratibu nzuri wa Utoaji na Usambazaji wa Zaka ni moja ya matatizo
yanayopelekea Zanzibar kuendelea kuwa na Watu wanaoishi katika
mazingira magumu na Umasikini uliopindukia.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Zaka na Sadaka Zanzibar (JUZASA) Shekh Said Suleiman
Masoud ameyasema hayo alipokuwa akitoa nasaha katika Mkutano wa Jumuiya
hiyo uliofanyika Ukumbi wa Shamtimba Kiembesamaki Zanzibar.
Amesema
Zanzibar kuna watu Wenye nafasi nzuri kiuchumi lakini wanashindwa
kutoa Zaka katika utaratibu Unaofaa na hivyo kushindwa kuwafikia
Walengwa wenye Mahitaji.
Amesema
Watu hao wenye uwezo wangekuwa wanatoa Zaka na kusambazwa katika
utaratibu unaofaa, Zanzibar ingekuwa haina Watu Masikini kutokana na
Zaka hizo kuwakomboa katika kiuchumi.
Sheikh
Said amesema wameamua kuanzisha Jumuiya ya (JUZASA) ili kurahisisha
Upatikanaji na Usambazaji wa Zaka baada ya kukosekana jambo hili kwa
miaka mingi.
Ameongeza
kuwa kwa muda mrefu Zanzibar kumeundwa Taasisi nyingi za Serikali na za
kibinafsi kwa ajili ya kumkomboa Mwananchi na Umasikini lakini malengo
yanashindwa kutimia kutokana na kukosekana Elimu ya Utoaji wa Zaka.
Kwa
upande wake Katibu wa Jumuiya ya JUZASA Omar Abubakar ameelezea Malengo
ya Zaka kuwa ni pamoja na Kuitakasa Mali ya Mtoaji na kumkomboa
Muislamu kutokana na Janga la Njaa.
Ametoa
wito kwa Waislamu kujitokeza kuwaunga Mkono sambamba na kupeleka Zaka
zao katika Jumuiya yao ili Waziwasilishe kwa walengwa wanaofaa kupewa
Zaka katika jamii.
Katika
Mkutano huo Jumuiya hiyo imefanya Uchaguzi ambapo Mwenyekiti wake na
Katibu wake wamechaguliwa tena kuiongoza Jumuiya hiyo kwa kipindi cha
miaka mitatu.
Jumuiya
hiyo iliyopata Usajili mwaka 2011 inapokea na kusambaza Zaka kwa
walengwa,ambapo malengo yake makuu ni kutekeleza vyema Suala la Zaka ili
kuweza kuwasaidia Wanajimii wanaoishi katika mazingira magumu na
umasikini uliokithiri.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR
Post a Comment