Hazina
ya fedha duniani IMF imesema kuwa haitatoa fedha zaidi kwa serikali ya
Zimbabwe kwa kuwa serikali hiyo ina madeni chungu nzima.
Kundi la
wataalam wa hazina hiyo barani afrika liko mjini Harare kukamilisha
mpango wa kuisadia serikali kuimarisha uchumi wake huku maelezo ya
mpango huo yakitarajiwa kutolewa wiki ijayo.
Naibu mkurugenzi wa
hazina hiyo anayesimamia Afrika Domenico Fanniza ,ameiambia BBC kwamba
utoaji wa mikopo mipya haupo katika mpango wao kwa sasa..
Bwana
Fanizza pia alionyesha wasiwasi wake kuhusu hatua ya serikali kutumia
robo tatu ya fedha za kodi kulipa mishahara ya takriban wafanyikazi laki
mbili na nusu wa serikali.
Post a Comment