Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa mtandao huu na kamanda wa polisi mkoa
wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani (pichani) askari hao waliofukuzwa kazi
ni EX.G. 3172 PC Ramadhani Iddi Saidi, EX.G. 9693 PC Emmanuel Morson
Lyimo pamoja na EX.G. PC Miraji Jumanne Mtea
Kamanda
Ngonyani amesema Jeshi la polisi limeamua kutoa adhabu hiyo kali
kutokana na vitendo mbalimbali vya utovu wa nidhamu walivyovifanya
ikiwemo tukio la hivi karibuni la kupigana hadharani Septemba 2 mwaka
huu Mjini Njombe
Amesema
wanategemea adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa askari wengine wenye tabia
kama hiyo kwani jeshi halitawavumilia askari wake ambao wanakwenda
kinyume cha sheria
Katika
hatua nyingine Kamanda Ngonyani amewataka wananchi kuwa makini na
askari hao waliofukuzwa kazi huku akisisitiza wananchi kutambua kuwa
askari hao si watumishi tena kuanzia Oktoba 24, mwaka huu
Na Edwin Moshi
Post a Comment