
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa yuko nchini Ethiopia kujadili mlipuko wa Ebola.
Ban
Ki Moon na Rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim Jumanne asubuhi,
wanakutana na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kuzungumzia mlipuko huo na
hali ya usalama katika mataifa ya pembe wa Afrika.Bwana Ban na Jim pamoja na mashirika mengine ya kimataifa, wako kwenye ziara, kutembelea nchi za Ethiopia, Kenya na Djibouti kuangalia masuala ya maendeleo na amani.
Tayari Umoja wa Mataifa na Benki ya dunia yametangaza ufadhili wa Dola bilioni nane, kusaidia mataifa hayo.
Post a Comment