BAVICHA YADAI TANZANIA INAONGOZWA NA MADALALI BADALA YA VIONGOZI

NA KENNETH NGELESI,eddy blog KYELA

LICHA ya Tanzania nchi na yenye rasilimali nyingi lakini ya Taifa masikini duniani na inashindwa kupiga hatua kimaendeleo kutokana na viongozi waliopewa dhamana ya kuingoza kujawa na ubinafsi na kwamba wakati  wote wanawaza uchaguzi na siyo matatizo ya wananchi.

Hayo yamebanishwa juzi na Makumu mwenyekiti baraza la vijana chama cha demokrasia na Maendeleo (Bavicha) Patric Ole Sosopi wakati akiwahutubia wananchi wa Kata Ipinda-Kyela, katika Mkutano wa haradhara wa kukijenga chama uliofanyika katika viwanja vya ghala la chakula mjini Ipinda.

Makamu huyo alisema kutokana na viongozi wengi kuwa wabinafsi na muda wote wanawaza uchaguzi, wanakosa nafasi ya kuwatumikia wananchi, na kwamba Tanzania inashindwa kupiga hatua kutokana na watu hao waliopewa dhamani kutokuwa uchungu, bali wengi wao ni madalali.

Sosopi alisema, hatua pekee ya kuondoka na viongozi wa aina hii ambao aliwaita madalali, ni kujiandikisha kwa wingi katika daftari la wakaazi ambalo lipo katika ofisi za maafisa watendaji wa kata, na daftari na kudumu la wapiga kura ili unapofika uchaguzi weweze kung’olewa kwa njia ya kura.

Akiwa hutubia mamia ya wananchi wa kata hiyo Sosopi alisema kuwa kushiriki kwa wingi katika Mikutano inayofanywa na chama hicho hakuna maana bali jukumu pekee ni kujiandikisha katika madaftari hayo ili zinapo fika chaguzi zote, Serikali za mitaa unao tarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani kuweza kuondoa Serikali ya kidhalimu ya chama cha mapinduzi.

‘Ndugu zangu wanaipinda na Kyela kwa ujumla, nchi hii hapigi hatua kimaendeleo kwani watu tulio wapa dhamani si viongozi bali ni madalali ambao wanawaza familia zao tu na ili kuondoka na watu hawa niwaombe likianza zoezi la uandikishaji katika daftari na wakazi,mjitokeze kwa wingi ili mshiriki vyema  chaguzi zote, Serikali za mitaa kwa maana ya Wenyeviti wa vitongoji,Vijiji na Mitaa kwa mijini ili  unapokuja uchaguzi Mkuu tuwang’oa hawa madalali’ alisema Sosopi

Aidha katika hatua nyingine Sosopi alisema kuwa viongozi wa CCM Chini ya aliye kuwa Mwenyekiti wa Bunge maalumu la Katiba Samwel Sita kuwa itakuwa ni historia kwani lilipofika zoezi la kupiga kura walipiga hata marehemu hatua aliyodai kuwa haijawahi kutokea popote duniani, hivyo ni halali kwa wafuasi wa chama cha mapinduzi kuita rasmi hiyo ni ya kihistoria.

‘Samwel Sita na wafuasi wa chama cha Mapinduzi wanajitapa eti? katiba itakayo patikana ni kihistoria hili ni sahihi kwani hakuna popote duniani isipo kuwa Tanzania tu ambapo hata marehemu waliokufa wanapiga kura  wakati wa kutafuta theluthi mbili ili kuungwa mkoni’ aliongeza Sosopi

Alisema kuwa kutokana na Serikali ya CCM chini ya Rais Kikwete kuupuza mawazo ya watanzania yalitolewa wakati wa Tume Jaji Joseph Warioba iliyopita kukusanya maoni ya wananchi lakini CCM imepuuza na kuamua kuweka mawazo ya kwao, alisema ni vema wananchi hao wakakaitaa rasmi hiyo kwa kupiga kura ya hapana wakati  utakapo fika wakati wa kupiga kura  ndiyo ama hapana.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa ni vema wananchi wakajenga utamaduni wa kuiadabisha Serikali tofauti alivyo sasa ambapo badala ya Serikali kuwaogopa wananchi ambao wameiweka madarakani lakini hali hiyo imegeuka wananchi wanaigopa hatua ambayo ni vigumu kwa taifa kupiga hatua.

naye Mwenyekiti wa baraza hilo Mkoa wa  Iringa Joseph Lyata, ambaye aliongozana na Makumu huyo aliwataka wananchi wa Kyela kumng’oa Mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM Dkt Harrison Mwakyembe kwa kile alicho kiita kiongozi huyo ni kigeugeu.

Alisema  Dk Mwakyembe ni kigeugeu ni kitendo cha waziri huyo kuyakana hata mawazo yake ambayo ni ya kitaalamu ambayo aliyafanyia tafiti, kuwa Tanzania ilihitaji muundo wa Serikali tatu lakini ulipofika wakati wa kujadili rasimiu iliyopendekezwa na tume ya Warioba DK Mwakyembe ameyakana, mawazo yake jambo ambalo ni hatari kwa kiongozi na kwamba ipo siku ataweza kuwa kana hata wananchi wake.

Aliongeza kuwa mbali na kujipambanua kuwa anapiga vita ufisadi katika Wizara aliyo pewa dhamana, ni vigumu kwa kiongozi huyo kufanikiwa kwani asilimia kubwa ya watu wanafanya ufisadi na kunufaika na Wizara hiyo ndiyo wadhamini wakuu wa chama cha Mapinduzi hiyo ni vigumu kufanikisha.

Lyata alisema DK Mwakyembe kamwe haiwezi Wizara ya Uchukukuzi kwani katika vitengo vyote vimeshikiliwa na wakubwa ambao kwa sehemu kubwa ndiyo wafadhili wa CCM ambapo ndiyo inayounda Serikali anayoiongoza.

Katika Mkutano huo ambao ulikuwa kwa ajili ya chama hicho viongozi hao wa Bavicha kuanzia ngazi ya kata hadi taifa kwa nyakati tofauti walisema Wilaya ya Kyela ambayo Dk Mwakyembe ni Mbunge wake haifanani na haiba aliyo nayo kwani amekuwa akipewa sifa kama kiongozi mpiganaji lakini wananchi pamoja na mazingira kwa ujumla hayafafani.

Akichanganua kauli hiyo Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa Joseph Kasambala alisema chama ccm  kimegawanyika katika vipande vitatu ambapo kipande cha kwanza ni kichwa ambao ni viongozi wa ngazi ya kitaifa,Tumbo ambao ni wakuu wa Wilaya Wakuu wa Mikoa na viongozi wa chama hicho, huku kipande cha mwisho ni Mkia ambao ni wananchi wanao yumbishwa wakiwa hawana hata mwelekeo huku wakiendelea kujinadi na kauli hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post