Ben Pol amesema kama Mungu akimjalia basi huenda akafunga ndoa na mpenzi wake Miss Tanzania namba mbili 2013, Latifa Mohamed.
Ben Pol amesema kuwa ukaribu alionao na Latifa unampa matumaini ya kudumu kwa uhusiano wao.
“Tupo karibu sana, suala la ndoa sijui nisemeje lakini, kama mwanaume
kamili tena kwa mila zetu nitaoa tu lakini, tukikubaliana na yeye
akawa tayari yaani kila mtu akiwa tayari na akili zetu zikiendana na
Mungu akijalia itakuwa hivyo. Pia unajua hii inakujaga automatic,”
amesema.
Katika hatua nyingine, Ben Pol amesema anatarajia kufanya video nyingine na Nisher.
“Huu upya ambao nakuja nao ni kuanzia uvaaji, yaani kuna mabadiliko
makubwa sana nataka kuja nayo ya kimwonekano. Ndioa maana nimeamua
kuachana na kufikiria kutoa wimbo redioni kwanza nataka kwanza video
moja tena kwa Nisher na haya mabadiliko yaambatane na wimbo mpya.”

Post a Comment