BREAKING NEWS: DODOMA, KONDOA WAPIGWA NA TETEMEKO USIKU HUU

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj-ZCpqRDWrXaIUjccyxvGeTul3lK6FfuIiOsW9rYwKm7A-4NUHA1GOWpf_Ph_0cUdi37HxwZKeIkXs1xRoIu17aNmI6G7Kq3XPNdzAa4NWfTRTZatKlrXThEYaAmhP_vZKIcvnwRe_VZbe/s400/r794151577.jpgMAENEO ya manispaa ya Dodoma na Kondoa yamepigwa na tetemeko la ardhi usiku huu.

Mtoa taarifa mkazi wa Dodoma maeneo ya Nkuhungu alisema kwamba tetemeko hilo lilitikisa mpaka makochi ambayo yamo katika majumba ya watu.
Ingawa Polisi hawajasema kitu, taarifa za kitaalamu kutoka katika tovuti inayoangalia matetemeko duniani na kutoa taarifa zake imethibitisha kutokea kwa tetemeko hilo majira ya  saa mbili na dakika 4 na sekunde 57 na nukta 6.
Aidha wamesema tetemeko hilo lilikuwa na nguvu ya Magnitude 5.1.Eneo lililokumbwa na mkasa huo linalopatikana kijiografia 5.41 Kusini (S) ; 36.01 Mashariki (E ) likiwa na kina cha kilomita mbili.
Kitovu chake kipo kaskazini mwa Dodoma  kiasi cha kilomita 89 na kiasi cha kilomita 62 Kusini Mashariki mwa Kondoa

Post a Comment

Previous Post Next Post