Thomas
Eric Duncan mwanaume aliesafiri kutoka Liberia mpaka Marekani akiwa
ameambukizwa virusi vya ugonjwa wa Ebola amefariki muda mfupi uliopita
nchini Marekani baada ya kuwa kwenye hali mbaya.
Pamoja na hayo pia mamlaka husika zinaendelea na jitihada za
kuhakikisha ugonjwa huo hausambai nchini humo na wanafahamu kabisa
kwamba virusi vya Ebola vinaweza kuishi kwenye miili ya watu waliofariki
ndio maana wakati wa kuizika ni watu pekee wenye mafunzo maalum tena
wakiwa wamejikinga ndio wanaruhusiwa.
Post a Comment