Mwaenyekiti wa zamani wa Simba,Hassan Dalali.
Na Nicodemus Jonas
HATIMAYE uongozi wa zamani wa Simba uliokuwa chini ya Hassan Dalali na Mwina Kaduguda, umetaka kuichukua timu hiyo kabla ya kuvaana na Yanga.
HATIMAYE uongozi wa zamani wa Simba uliokuwa chini ya Hassan Dalali na Mwina Kaduguda, umetaka kuichukua timu hiyo kabla ya kuvaana na Yanga.
Simba na Yanga zinatarajiwa kuvaana Oktoba 18 kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa timu hizo kukutana
msimu huu.
Habari za ndani ambazo zimelifikia Championi Jumatano zinasema kuwa,
uongozi huo chini ya Dalali unataka kuichukua timu hiyo kwa ajili ya
maandalizi ya mechi hiyo baada ya kuona mwenendo wa timu hiyo siyo
mzuri.
“Kina Dalali wana historia nzuri sana ya kuifunga Yanga, mara kwa
mara wamekuwa wakiibuka na ushindi kama sikosei waliwahi kupoteza mechi
moja tu dhidi ya Yanga.“Naona sasa wanataka kuongeza nguvu kwa kuwa
wameomba wakabidhiwe timu wakiwa na viongozi ambao wapo madarakani chini
ya Evans Aveva ili wafanye maandalizi wote.
“Wenyewe wanasema ni kwenye mechi zote zilizobaki za Ligi Kuu
Tanzania Bara lakini inafahamika kuwa shida yao kubwa ni kuona Simba
wanaifunga Yanga,” kilisema chanzo hicho.Hata hivyo, baada ya kupata
taarifa hizo, Championi Jumatano lilimtafuta Dalali ambaye aliwahi
kuiongoza Simba iliyomaliza msimu bila kufungwa ambapo alifunguka:
“Aah ishu siyo Simba na Yanga tu, unajua sisi bado ni viongozi,
tuliandika yale ambayo tunaona yanafaa kwa ajili ya Simba tukiwa
viongozi wote wakati wa uongozi wangu tukapeleka kwa viongozi wa sasa.
“Lakini sanasana tulitaka kukutana na viongozi wa sasa ili tujadili
pamoja kuhusu muenendo wa timu ulivyo, unajua hapa kabla ya Yanga ndiyo
kuna muda mrefu kidogo, hivyo tuliona tukikaa hapa tunaweza kujadiliana
vizuri zaidi.
“Naomba tu kila mtu aelewe hivyo, mimi nipo kwenye Bodi ya Udhamini
ya Simba, hivyo siwezi kuzungumza zaidi,” alisema Dalali.Hata hivyo,
Katibu Mkuu wa Simba katika uongozi wa Dalali, Mwina Kaduguda ‘Simba wa
Yuda’, alisema wameamua kuomba kukutana na viongozi walio madarakani
kutokana na homa ya mchezo huo.
“Tulitoa mapendekezo yetu kama viongozi wa zamani kutaka timu yetu
iimarishwe, lakini pia tumewaomba tuketi meza moja, tubadilishane mawazo
katika mchezo wa Yanga. Simba ni yetu na kila mmoja anahitaji kuona
Simba inazidi kufanya vema dhidi ya Yanga, ndiyo maana tumewaomba
kukutana nao,” alisema Kaduguda
Post a Comment