Kasi
kubwa ya usaambaji wa virusi vya ugonjwa wa Ebola imesababisha michuano
ya kombe la mataifa ya Africa mashakani na hivyo kuahirishwa mpaka
mwakani.
michuano hiyo ilipaswa kupigwa katika nchi ya Morocco
mnamo tarehe kumi na saba ya mwezi wa kwanza,na serikali ya Morocco
iliwaambia waandaaji ya kwamba inataka kuahirisha michuano hiyo sababau
ya kasi ya ugonjwa huo.
Serikali hiyo imezingatia hatari
iliyowekwa wazi na mashabiki kutoka katika nchi za Africa Magharibi.nayo
bodi ya utendaji inayoongozwa na shirikisho la soka barani Africa CAF
inatarajiwa kufanya maamuzi yake ya mwisho mwezi ujao,
ingawa mpaka sasa shirikisho hilo limebaki na msimamo wake kwamba michuano hiyo iendelee kama kawaida.
Post a Comment