Kundi la Friends of Simba
Na Mwandishi WetuKUNDI la Friends of Simba (Fos) limetoa kitita cha Sh milioni 25, kwa ajili ya kambi ya Simba nchini Afrika Kusini.
Habari za uhakika kutoka Afrika Kusini zimeeleza kuwa Fos walitoa fedha hizo ili zitumike kwa ajili ya kambi hiyo.
Chanzo cha uhakika kutoka Simba kimeeleza Fos walitoa fedha hizo na nusu zilitolewa na uongozi wa Msimbazi.“Kambi ya Afrika Kusini imetumia jumla ya Sh milioni 52, kwa ajili ya nauli na kambi kama chakula, usafiri wa ndani na mambo mengi, lakini inaweza kuzidi.
“Friends wenyewe walitoa fedha milioni ishirini na tano, ikatumika kwa nauli kuja huku, pia kurudi nyumbani.
“Wako hapa baadhi yao wamekuwa wakitoa motisha kwa wachezaji ili kuimarisha kikosi, si kwa ajili ya mechi ya Yanga tu, ligi nzima,” kilieleza chanzo.
Kuhusu hilo, mmoja wa viongozi wa Fos, Kassim Dewji, aliye nchini Afrika Kusini, alithibitisha hilo, lakini akakataa kutaja idadi.“Kweli Friends wametoa fedha baada ya kujichangisha, hii ni kawaida wajumbe wake kufanya hivyo hata wanapokuwa nje ya timu kwa lengo la kusaidia, hii inatokana na mapenzi yao kwa Simba.
“Uongozi pia umetoa fedha kufanikisha hili, lakini sidhani kama ni sahihi kuanza kusema viwango kwenye vyombo vya habari,” alisema Dewji.Simba itacheza mechi yake ya mwisho ya kirafiki leo dhidi ya SuperSport, kabla ya kurejea nchini.
Post a Comment