
Mwanasheria
Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman akipiga kura leo kwenye
ukumbi wa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma kupitisha Sura na Ibara za
Rasimu ya Katiba inayopendekezwa.

Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Yahya Kassim Issa akiomba mwongozo leo
Bungeni kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta
kuhusu kitendo cha Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud
Othman kuja kupiga kura na kukataa baadhi ya Ibara za Rasimu ya Katiba
inayopendekezwa wakati alijitoa kwenye Kamati ya Uandishi ambapo
alitakiwa awepo akitetea maslahi ya Zanzibar, jambo ambalo
limewachanganya baadhi ya wajumbe.

Mwanasheria
Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman akisindikizwa kutoka ndani
ya ukumbi wa Bunge Maalum leo mjini Dodoma na Askari Polisi.

Mwanasheria
Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman (mwenye Kaunda suti ya
kijivu) akisindikizwa kutoka nje ya viwanja vya Bunge Maalum la Katiba
leo mjini Dodoma na Askari Polisi mara baada ya kushutumiwa na baadhi ya
Wajumbe wa Zanzibar.

Wajumbe
wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Mzee Kingunge Ngombale Mwiru pamoja
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella
Mukangara wakibadilishana mawazo kwenye viwanja vya bunge hilo mjini
Dodoma leo.

Waziri
Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe.
Mizengo Pinda (wa pili toka kulia) akibadilishana mawazo kwenye viwanja
vya bunge hilo mjini Dodoma leo na wajumbe wenzie wa bunge Maalum la
Katiba. Wajumbe hao ni, Mhe. John Shibuda (kulia), Mhe. Mzee Kingunge
Ngombale Mwiru (wa pili kushoto) na Mhe. Sophia Simba (kushoto).


Waziri
Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe.
Mizengo Pinda (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na mjumbe mwenzie wa
bunge hilo, Mhe. Sophia Simba.(Picha zote na Benedict Liwenga,
Maelezo-Dodoma).
Post a Comment