HILI NDILO KUBWA WALILOKUBALIANA CHADEMA KWENYE MKUTANO WA KAMATI KUU ULIOMALIZIKA

Katibu mkuu wa Chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA dk WILLBROD SLAA akizingumza na wanahabari jijini Dar es salaam mapema leo
Chama cha democrasia na maendeleo chadema leo kimetagnaza rasmi kuanza kwa kampeni ya siku ishirini nchi nzima ya kuzunguka kuwahamasisha watanzania kuipinga kwa nguvu moja rasimu ya katiba iliyopendekezwa na bunge maalum la katiba kwa kile walichooita kuwa ni kukosa uhalali wa kisheria na kujawa na ukiukwaji mkubwa wa kisheria tangia mchakato huo kuanza.


Akizungumza na wanahabari jijini dar es salaam wakati akisoma maadhimio ya kamati kuu ya chama hicho katibu mkuu wa CHADEMA dk WILBROD SLAA amesema kuwa kamati kuu imejiridhisha kuwa mchakato wa katiba katika hatua zake zote ulitawaliwa na nia mbaya iliyokuwa na lengo kuu la kuhakikisha kuwa hakuna mabadiliko makubwa na ya maana yatakayofanyika kwenye mfumo wa kikatiba na kiutawala ambao umekuwepo nchini kwa miaka zaidi ya hamsini.

Dk slaa amesema kuwa mkutano huo uliokaa kwa siku mbili jijini Dar es salaam umekuja na maadhimio mengi lakini kubwa likiwa ni kuwahamasisha wananchi kupiga kura ya hapana kwa katiba pendekezwa pamopja na kuwahamasisha kujitpokeza katika chaguzi za serikali za mitaa zitakazokuja.

Akitaja mambo ambayo yameufanya mchakato wa katiba kutokuwa na uhaali kwao ni pamoja na uteuzi wa wajumbe ambao wengi amesema walichaguliwa kwa lengo la kuwasaidia ccm,lugha chafu ndani ya bunge,bunge maalum la katiba kugeuzwa tume na kuanza kukusanya maoni upya,muda wa kuwasilishwa kwa taarifa na kamati mbalimbali ulifupishwa,utaratibu wa kupiga kura kifungu kwa kifungu ulibadilishwa,pamoja na wajumbe waliokuwa nje ya bunge kupiga kura.


Kutokana na mambo hayo chama hicho kimeamua kwenda nchi nzima kuwahamasisha watanzania kupiga kura ya hapana kwa mchakato huo ambapo wanaenda kwa mafungu ambapo kesho baraza la wanawake BAWACHA wanaanzia MWANZA na baadae kufwata baraza la vijana na wengine.

Post a Comment

Previous Post Next Post