Waziri wa Maji, Prof.
Jumanne Maghembe na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,
Mifugo na Maji, Prof. Peter Msolla wakiwa kwenye kiwanda cha nyama ya
kuku wakiangalia utendaji na uendeshaji wake.
Mjumbe wa Kamati, Prof. David Mwakyusa akiangalia moja ya kifaa cha kisasa katika Hospitali ya Mji wa Merowe.
Mtambo wa kuzalisha umeme katika Bwawa la Merowe.
Ujumbe wa Tanzania,
viongozi wa Sudan na wataalam mbalimbali wa Bwawa la kuzalisha umeme la
Merowe wakiwa katika picha ya pamoja katika bwawa hilo.
Ndani ya jengo la bwawa la kuzalisha umeme la Merowe.
Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imetembelea Bwawa la Kuzalisha Umeme la
Merowe katika Mji wa Merowe na kujionea namna ya wenyeji wanavyotumia
maji ya Mto Nile kwa kuzalisha umeme wa kutosha kwa ajili ya mji huo na
nchi nzima ya Sudan.
Mradi wa Bwawa la
Merowe ni mkubwa katika nchi ya Sudan na mbali na kuzalisha umeme, pia
unatumika kwa shughuli za kilimo cha umwagiliaji ambacho kwa aslimia mia
kinategemea Mto Nile.
Aidha, mradi wa bwawa
hilo pia umechangia kuleta maendeleo makubwa kiuchumi kwa kuwezesha
kujengwa kwa uwanja bora wa ndege wa kisasa, hospitali bora ya kisasa na
kiwanda kikubwa cha nyama ya kuku katika mji wa Merowe.
Hivyo, kuonyesha
jinsi gani nchi ya Sudan inavyotumia fursa ya maji ya Mto Nile vizuri
katika kuleta maendeleo ya Sekta zote nchini mwao.
Hii ni muendelezo wa
ziara ya siku nne nchini humo kwa kamati hiyo, katika kujifunza namna ya
kutumia vizuri rasilimali ya maji ya Mto Nile katika kukuza maendeleo
ya nchi.
Post a Comment