KAMBANGWA WAENDELEA KUNUFAIKA NA MRADI WA KOMPYUTA WA VODACOM



Wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari yaKambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar esSalaam,wakioneshwa na Meneja miradi na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza moja ya progamu zinazopatikana katika Kompyuta zinazowawezesha kupata taarifa ya masomo mbalimbali kwa njia ya mtandao wakati alipotembelea shuleni hapo kwa ajili ya kujua maendeleo ya mradi wa TEHAMA uliofadhiliwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Samsung.Zaidi yawanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.



Mwalimu Mkuu wa Shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam Theresia Ng’wigulu (kulia) Meneja miradi na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza (kushoto ) pamoja na Meneja uhusiano wa umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (katikati) wakimsikiliza mmoja wa wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Kambangwa, Matha Galusaki akielezea jinsi anavyoweza kupata taarifa za masomo mbalimbali kwa njia ya mtandao, wakati walipotembelewa na maofisa wa Vodacom shuleni hapo kujua maendeleo ya mradiwa TEHAMA  uliofadhiliwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Samsung. Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.(P.T)
Baadhi ya Wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Theresia Ng’wigulu watatu toka kulia pamoja na maofisa wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu wa kwanza kushoto na Renatus Rwehikiza (kulia) wakimsikiliza Mwalimu wa somo la kompyuta wa kidato cha pili Nicolas Wilson wa shule hiyo akiwafafanulia jambo kuhusiana na elimu ya mafunzo ya kompyuta wakati walipotembelewa na maofisa hao kujua maendeleo ya mradi wa TEHAMA  uliofadhiliwana Vodacom Foundation  kwa kushirikiana na Kampuni ya Samsung. Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.

Post a Comment

Previous Post Next Post