Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi waliofika kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Tangamano kata ya
Tangamano wilaya ya Tanga mjini.
Wananchi wakiwa
na bango lao kwenye mkutano wa hadhara wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu
wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa mikutano Tangamano.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana , Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye kwa pamoja wakiwapungia wananchi waliofika kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mikutano Tangamano, Tanga mjini.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipeana mkono na Mzee Athumani Makalo
wakati akiwasili kwenye uwanja wa mkutano wa Tangamano.
Wananchi wa Tanga mjini wakishangilia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM kwenye viwanja hivyo ya mikutano.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wote waliohudhuria mkutano kwa kuwapingia mikono yote miwili.
Wananchi nao hawakuwa nyuma kumpungia kiongozi wao.
Mkuu wa wilaya
ya Tanga mjini Mh.Halima Dendegu akiwasalimia watu waliofurika uwanjani
kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Kila mwananchi wa tanga alikuwa na shauku ya kusikiliza mkutano huo
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwapungia mkono maelfu ya watu
waliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye uwanja wa Tangamano.
Wananchi
wakishangilia kwa nguvu wakati wa hotuba ya Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye akihutubia kwenye uwanja wa Tangamano
Wadau wa CCM mkoa wa Tanga wakifuatilia mkutano
Kila mtu wa Tanga alikuwepo kwenye mkutano huo.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Tanga mjini na
kuwaambia watendaji wa serikali kutoka maofisini na kwenda kwa wananchi
ambao wanamaswali ya matatizo yao na wanahitaji majibu.
Mwenyekiti wa UWT
mkoa wa Tanga Mama Aisha Kigoda pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tanga mjini
Mh.Halima Dendegu wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi kwenye
mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
uliofanyika kwenye viwanja vya Tangamano.
Mbunge wa Jimbo
la Tanga mjini Mh.Omari Nundu akihutubia wananchi wa Tanga mjini kwenye
mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Tanga mjini ambapo
aliwaambia muda wa kuwaambia watanzania maendeleo yapo kwenye mipango
umekwisha na kutaka viongozi kutimiza wajibu wao.
Maelfu ya wakazi
wa Tanga wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
alipokuwa anahitimisha ziara yake ya siku 11 kwenye mkoa wa Tanga.
Wananchi
wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
ambapo pamoja na yote alizungumzia uchumi wa Tanga ambapo aliwaambia
wananchi hao lazima reli na bandari zifanye kazi ili uchumi wa mkoa wa
Tanga ubadilike.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisitiza jambo wakati akihutubia wakazi wa Tanga mjini.
Katibu Mkuu wa CCM akiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama waliojiunga na CCM kutokea chama cha CUF
Mzee Athumani
Makalo akitoa salaam za pongezi kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwa hotuba nzuri
zilizobadilisha siasa ya Tanga .
Mzee Makalo akimvisha Katibu Mkuu joho zawadi kutoka kwa wazee wa Tanga mjini.
Katibu Mkuu wa CCM akiagana na watu baada ya kumaliza mkutano
Watu wakigombania kumshika mkono Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akiondok kwenye uwanja wa mikutano
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wananchi kama ishara ya
kuwaaga baada ya kumaliza mkutano mkubwa mjini Tanga.
Kila mtu alimuaga Katibu Mkuu wa CCM kwani mkutano wake wa leo aliongelea masuala ya msingi yanayohusu mkoa wa Tanga.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Post a Comment