Mwanamke mmoja Kilimanjaro amekamatwa na
polisi akidaiwa kumkata mtoto wake mwenye umri wa miaka nane nyama ya
paja na kuichoma mithili ya mshikaki.
Mwananmke huyo aliyetajwa kwa jina la
Dafrosa Massawe anadaiwa kufanya unyama huo mwishoni mwa wiki na
majirani wanasema mama huyo alifanya hivyo akiwa amelewa.
Kamanda wa Polisi Kilimanjaro Koka Moita
alisema mwanamke huyo ataendelea kushikiliwa hadi uchunguzi wa tuhuma
hizo utakapokamilika kabla ya kupelekwa mahakamani.
Akizungumza na Gazeti la MWANANCHI
katika hospitali ya Kibosho mtoto huyo alisema hafahamu kosa alilofanya
hadi mama yake ambaye ni mtengenezaji wa pombe za kienyeji kumfanyia
kitendo hicho.
Alisema mama yake alirudi nyumbani usiku
na kumkuta amekaa na kumsalimia kisha akamwomba chakula wakati akijua
hakuna na baadae aliingia jikoni na kuchukua kisu kisha kumkata nyama
kwenye paja lake baada ya kumwambia alishinda na njaa siku nzima.
Alisema baada ya kuikata aliichoma kama
mshikaki na ilipoanza kufuka moshi na kutoa harufu aliitoa jikoni na
kumwekea mtoto huyo puani ili avute harufu yake.

Post a Comment