Serikali ya Tanzania imepiga marufuku uingizaji wa mfuko ya plastiki
kutoka nje ya nchi kutokana na kuendelea kwa uzembe na kuingiza bidhaa
zilizo chini ya viwango kinyume cha sheria ya uhifadhi wa mazingira na
maazimio ya Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Mhe. Bilinith Mahenge ameyasema hayo hapo jana jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushitukiza katika makampuni yanayotengeneza, kuagiza na kuuza mifuko hiyo kutoka nje ya nchi.
Ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge la 10 na Sheria ya uhifadhi wa mazingira.
Kwa upande wao, watengenezaji, waagizaji na wauzaji pamoja na kumpongeza Waziri kwa hatua yake ya kuwatembelea, waliwashutumu tabia ya baadhi ya Watendaji kwa kutokuwashirikisha katika mambo mbalimbali ya sheria na mikakakti kama wadau. Wamesema jambo hilo linaweza kuchangia uduni wa biashara baina yao na Serikali na kusema wapo tayari kutimiza bila kikwazo endapo watashirikishwa kikamilifu.

Post a Comment