Najua
kama umekua karibu na simu yako leo mitandao ya kijamii hasa Whatsap na
twitter inaweza kuwa imetumika kukufikishia Taarifa zilizoanza
kuzungumziwa na watu mbalimbali saa kadhaa zilizopita kwamba msanii Chid
Benz amekamatwa na Polisi.
Taarifa zinasema kakamatwa na Polisi
kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam akiwa anaelekea Mbeya na hiyo
imetokea baada ya kukutwa na vitu ambavyo ni kosa kwa yeyote kukutwa
navyo.
Wakati tunaendelea kufatilia hii taarifa kwa upande wa pili wa Polisi,
tumezungumza na muandaaji wa show ya Instagram Party ambayo Chid Benz
ndio alikua anakwenda kushiriki kesho.
Fred amekiri kweli Chid Benz amezuiliwa na Polisi kwa kukutwa na vitu ambavyo hajavifahamu >>> “Sijapewa
taarifa kamili lakini naambiwa kuna tatizo limetokea airport ya Dar es
Salaam akiwa anasafiri kuja Mbeya, wameniambia kuna vitu ambavyo amebeba
haviruhusiwi kupita Airport“
Chidi Benz alikua ameongozana na msanii
mwenzake ambae ni Shetta hivyo Chidi kabaki na Polisi na Shetta
amekwenda kupanda ndege kwa ajili ya kuelekea Mbeya.
tunaendelea kufatilia zaidi hizi taarifa ili kupata uhakika kutoka kwa upande wa Polisi.
Post a Comment