Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Watu wa China Ndugu Li Yuanchao wakati walipokutana kwenye Sherehe ya
kutimiza Miaka 50 ya Uhusiano wa Kidiplomasia baina ya Tanzania na
China. Sherehe hizo zilizoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini China
na kufanyika jijini Beijing leo.
Makamu
wa Rais wa China Ndugu Li Yuanchao akigonganisha glasi na Mama Salma
Kikwete ikiwa ni ishara ya kusherehekea kutimiza miaka 50 ya ushirikiano
wa kidiplomasia kati ya Tanzania na China. Sherehe hizo zilifanyika
jijini Beijing.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akigonganisha glasi na Mkewe Mama Salma
wakisherehekea kutimiza miaka 50 ya ushirikiano wa Kidiplomasia kati ya
Tanzania na China.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Ndugu Bernard Membe wakisherehekea kutimiza miaka 50 ya
Ushirikiano wa Kidiplomasia baina ya Tanzania na Cina kwa kugonganisha
glasi zao huku Mama Salma na Makamu wa Rais wa China Ndugu Li Yuanchao
(aliyesimama kulia) wakishuhudia. Sherehe hizo zilifanyika Beijing
nchini China leo. (PICHA NA JOHN LUKUWI).
Post a Comment