Video:- Msanii wa Kenya atumia tshs milioni 12 kukodi helikopta kuhudhuria hafla za mwanae na mdogo wake, Nairobi na Eldoret kwa siku 1

Muimbaji wa Kenya, Esther Akoth maarufu kama Akothee ambaye hivi karibuni alikuwa nchini Tanzania, ametumia shilingi 700,000 za Kenya ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 12 za Tanzania kuhudhuria hafla mbili ikiwemo ya mwanae wa kike zilizofanyika siku moja.
IMG-20141003-WA0004 Esther Akoth aka Akothee akiwa kwenye helikopta aliyokodi
Akothee ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Akothee Safaris: Tours & Travel ya Mombasa, Kenya ameiambia Bongo5 kuwa imemlazimu kutumia gharama hiyo kwakuwa hakutaka kukosa hafla hizo zilizofanyika leo katika miji tofauti, Eldoret na Nairobi nchini humo.
IMG-20141003-WA0005
“Sikuwa na namna lakini imenilazimu kuhudhuria hafla zote bila kuumiza hisia za mwanangu Prudence Vanpelt ambaye yupo Utawala Academy Nairobi na pia kukosa mahafali ya mdogo wangu Moi University, Eldoret,” amesema.
IMG-20141003-WA0006 Akothee na meneja wake
“Bila kusahau kazi yangu na mapenzi katika muziki, natakiwa kurejea Nairobi kesho (Jumamosi) kufungua show ya Chameleone kwenye party ya huko Athi River, Nairobi.”
Akothee amesema rubani wa helikopta hiyo ndiye aliyembeba Akon wakati akiwa Kenya. Mfahamu zaidi msanii huyo kwa interview aliyofanya na Bongo5 hivi karibuni.

Post a Comment

Previous Post Next Post