Rais Uhuru Kenyatta akiwasili katika mahakama ya kimataifa ya ICC
Idadi
kubwa ya wabunge nchini Kenya wanajiandaa kuandamana na Rais Uhuru
Kenyatta katika mahakama ya kimataifa ya ICC,Uholanzi ambako anatarajiwa
kuhudhuria kikao maalum kuhusiana na kesi inayomkabili katika mahakama
hiyo.
Kenyatta ametakiwa kufika mbele ya mahakama hiyo tarehe nane
mwezi huu huku kiongozi wa mashitaka Fatou Bensouda akilalamika kuwa
Kenya imekataa kushirikiana na mahakama hiyo kuhusiana na ushahidi dhidi
ya Kenyatta.
Mapema wiki hii, mahakama hiyo ya ICC ilitupilia
mbali ombi la Rais Kenyatta, la kutaka kikao hicho cha Octoba 8
kuhairishwa au aruhusiwe kutumia video. Majaji wa Mahakama hiyo
walimuagiza Uhuru kufika binafsi mbele yao.
Wabunge hao walifika
mmoja baada ya mwingine na kupanga foleni ndefu kuanzia asubuhi kuomba
viza huku baadhi yao wakidai kuwa takriban wabunge 100 tayari
wamewasilisha maombi ya visa kusafiri Uholanzi.
Wengi wa
waliowasilisha maombi yao Ijumaa, walikuwa kutoka upande wa serikali.
Lakini mwandishi wetu wa BBC Emanuel Igunza alizungumza na Mbunge wa
Upinzani Jenerali Joseph Nkaiserry ambaye pia atasafiri pamoja na Rais.
''Suala
hili sio la mrengo mmoja wa bunge au mwingine. Rais ni kiongozi wa
Kenya nzima na ingepaswa sisi sote kama watoto wa chi hii kuwa pamoja na
yeye’ alisema Nkaiserry ambaye ni mbunge wa upinzani.
Mbunge wa
Lagdera, Kaskazini Mashariki mwa Kenya Mohammed Shidiye alisema kesi
hiyo ya ICC, sio swala la Kibinafsi kwa rais bali ni la kitaifa
''Tunaona
kwamba rais wetu anadhulumiwa, taifa letu linadhulumiwa na shida
zimekuwa nyingi sana, kesi hii ni mambo ya kuwadanganya Wakenya,''
aliongeza Shidiye
Msemaji wa rais hata hivyo alikataa kuithibitishia BBC iwapo Uhuru Kenyatta atasafiri kuelekea Hague.
Kenyatta
anatuhumiwa kuhusika na kupanga ghasia za kikabila zilizosababisha vifo
na kuwalazmisha maelfu ya watu kutoroka makwao kwa hofu ya
kushambuliwa.
Kenyatta amekanusha madai hayo dhidi yake.
Yote
hayo yalitokea baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007 uliozua ubishi katika
ya serikali na upinzani kuhusu mshindi halisi wa uchaguzi huo
ulioshindaniwa na aliyekuwa Rais Mwai Kibaki na kiongozi wa upinzani
Raila Odinga.
Post a Comment