Wafanyakazi wa TIGO washiriki matembezi ya kuchangia fedha kwa ajili ya Saratani ya matiti jijini Dar


3
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akisalimiana na Meneja wa huduma za Jamii wa kampuni ya simu ya Tigo, Woinde Shisael (kulia) kabla ya kuanza kwa matembezi ya kuchangia fedha kwa ajili ya Saratani ya matiti jijini Dar es Salam jana yaliyodhaminiwa na kampuni hiyo. Wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya saratani ya Ocean Road, Diwani Msemwa (kushoto kwake) na Mkurugenzi wa Wellworth Tanzania, Saul Basckin.
1
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akifanya mazoezi kabla ya kuanza matembezi ya kuchangia fedha kwa ajili ya Saratani ya matiti jijini Dar es Salam jana, Matembezi hayo yaliyodhaminiwa na kampuni ya simu ya Tigo.
8
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii ,Dk. Seif Rashid akiongea na watu waliohudhuria matembezi ya hisani ya kuchangia fedha kwa ajili ya saratani ya matiti Kunduchi Beach Hotel.
7
Meneja wa huduma za Jamii wa kampuni ya simu ya Tigo, Woinde Shisael akiongea na watu waliohudhuria matembezi ya hisani ya kuchangia fedha kwa ajili ya saratani ya matiti Kunduchi Beach Hotel.
5
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (wa tatu kushoto) akiongoza matembezi ya kuchangia fedha kwa ajili ya Saratani ya matiti jijini Dar es Salam jana yaliyodhaminiwa na kampuni ya simu ya Tigo. Kulia ni Meneja wa huduma za Jamii wa kampuni ya simu ya Tigo, Woinde Shisael na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya saratani ya Ocean Road, Diwani Msemwa (kushoto kwa waziri).
10
Wafanyakazi wa kampuni ya Simu za mkononi Tigo wakipozi kwenye picha ya pamoja baada ya matembezi ya kuchangia fedha kwa ajili ya Saratani ya matiti jijini Dar es Salam.
11
12

Post a Comment

Previous Post Next Post