Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) limezungumzia sakata la maaskofu wa kanisa hilo, Methodius Kilaini na Eusebius Nzigirwa kudaiwa kupewa fedha za akaunti ya Tegeta Escrow na kusema kwa sasa hawawezi kuzungumzia suala hilo kutokana na kuwa linagusa watu binafsi.
Limesema
kuwa suala hilo halihusu baraza na inaweza kufanyiwa kazi kwa taratibu
za kanisa kwa kadri uchunguzi unavyoendelea kufanyika, lakini sasa ni
mapema mno.
Msemaji wa Baraza hilo, Padri Anatoly Salawa alisema
kwa sasa suala hilo wazungumzaji ni watu binafsi ambao wanahusika katika
sakata hilo na siyo kama baraza.
Alisema orodha inawahusu watu
wengi na kwamba wakati mwafaka ukifika kanisa litatoa kauli, lakini
suala hilo ni binafsi na askofu yeyote ana haki ya kufungua akaunti
binafsi kama ilivyo kwa mtu yeyote.
Alisema suala hapo linalohusu
kanisa ni Benki ya Mkombozi, lakini hata hivyo benki haina mamlaka ya
kumuuliza mteja alipopata fedha mpaka watilie shaka na kutoa taarifa
Benki Kuu ili kuchunguza.
Padri Salawa alikana taarifa
zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa Askofu Msaidizi wa Kanisa
Katoliki Bukoba, Methodius Kilaini aliitwa jijini Dar es Salaam kutokana
na tuhuma hizo.
“Taarifa hizo siyo za kweli, kwani Askofu
Kilaini yupo hapa jijini Dar es Salaam kufungua kongamano la kiroho la
Afrika Mashariki alilofungua jana (juzi) katika ukumbi wa Baraza la
Maaskofu na mpaka sasa bado yupo,” alisema.
Post a Comment