Said Fella amedai kuwa na mipango ya kuzungumza na Juma Nature ili waanze tena kufanya kazi pamoja.

Fella aliiambia 255 ya XXL, Clouds FM kuwa kuna kila sababu ya kuweka
mambo sawa na msanii huyo nguli maisha ya kazi yaendelee kama zamani.
“Huo ni mapango wangu mimi, kwa sababu mimi ndo nafikiria, kama
ilitokea wakati ule misunderstanding, kama tulishawishiwa ili tusifanye
kazi bana imefika wakati lazima kusameheana,” alisema Fella.
“Mimi nimefikiria nimeona nitakaa na mwanangu nimfahamishe jinsi gani
tufanye kazi ili na yeye arudi tufanye kazi. Kuongea tunaongea na mambo
muhimu tunashirikiana ila kwenye suala la kazi ndo hilo kwamba
nimefikiria ni lazima Mheshimiwa Temba, Chege, na yeye Juma Kassim
Kiroboto lazima wakae pamoja wafanye ngoma moja kwanza,” aliongeza.
Fela alidai kuwa chanzo kikubwa cha ugomvi kati ya Nature na wasanii wengine wakiwemo Temba na Chege ni mwanamke.
“Tatizo wote tulivurungwa na ujana mwisho wa siku tukatoa chance kwa
watu na wamechukua nafasi. Siwezi kusema sio au ndio, lakini huyo
mwanamke ameshinda ametushawishi mpaka kubomoa, maana yake ni sawa
sawa mwanamke anatumwa kwenda kubomoa nchi. Viongozi kama tunagombania
nchi kwaajili ya mwanamke basi tulifeli sisi upande wetu,” alisisitiza.
Bongo5 ilimtafuta Nature kutaka kujua kama yupo tayari kufanya kazi na Fella na kudai kuwa amesikia taarifa za mpango huo.
“Siwezi kusema tunaweza tukafanya kazi au hatutafanyam,” amesema
Nature. “Mimi bado sijaongea naye lolote labda mwenyewe ameamua kusema
hivyo ilimradi kionekane ni kitu kizuri. Mimi bado nasikia sikia kwamba
Fella kaongea hivi na hivi lakini mimi sijasikia na hajanifuata mimi
kuniambia habari hizo. Siwezi kulizungumzia kwa sababu litakuwa
linanichota mawazo yangu wakati yeye mhusika hajaniijia.”
Post a Comment