Google washtakiwa, Watakiwa kuondoa taarifa zenye kuchafua hali ya hewa

SHAURI la Muingreza mmoja dhidi ya mtandao wa Google , anayetaka mtandao huo kuzuia na kuondoa taarifa zake zilizoingizwa na watu wasiojulikana zenye kumuudhi na kumletea picha mbaya katika jamii inaanza katika mahakama kuu ya London, Uingereza.
Muingereza huyoDaniel Hegglin amesema katika taarifa hizo amekuwa akituhumiwa yeye kama muuaji,anayewadhalilisha watoto na shabiki wa kundi la wabaguzi la Ku Klux Klan.
Muingerza huyo anaitaka Google kuzuia posting hizo  kuonekana au kuingia katika hifadhi ya Google.
Aidha katika shauri hilo Google nao wamemtaka atoe orodha ya linki anazotaka ziondolewe, ingawa Mahakama Kuu inatarajiwa kusema kama injini hiyo katika mtandao wa kompyuta inatakiwa kufanya zaidi.
Hegglin, ambaye kwa sasa anaishi nchini Hong Kong, awali alikuwa anaishi na kufanyakazi mjini London, Uingereza na alitambua kuwapo kwa taarifa hizo mbaya dhidi yake katika mtandao mwaka 2011.
Amedai Muingereza huyo kwamba kuna zaidi ya webu 3,600 zenye taarifa zake ambazo si za kweli na zenye kuudhi na amesema kwamba kuorodhesha  zote kwa ajili ya Google kuzifanyia kazi zitakuwa ni gharama kubwa, kupoteza wakati na haitasaidia.
Amesema ingawa Google sio wenye asili na taarifa hizo, injini zake zimewezesha kusambaa kwa taarifa hizo, na hivyo anataka mahakama kuilazimisha Google kuchukua hatua kuzuia tarifa hizo kupatikana  England na Wales.

Mchambuzi wa masuala ya sheria wa Shirika la Utangazaji la Uingereza(BBC), Clive Coleman  amesema shauri hilo si shauri la kusahaulika kwa kuwa linagusa usambazaji na uchapishaji wa taarifa zenye kuudhi na ambazo si za kweli katika mtandao wa kompyuta.

Aidha amesema  shauri hilo limelenga kuangalia ukweli kwamba mtu yoyote anaweza kuposti kitu chochoite cha kuudhi au kumharibia jina mtu mwingine katika mtandao huku akizuia anuani yake kuonekana.
Shauri hilo litakalosikilizwa katika mahakama kuu ya London limeelezwa kuwa shauri la msingi litakalokuwa na  athari kubwa katika mwenendo wa injini za habari na wananchi wanaotumia.
Aidha shauri hilo linafanyika wakati mahakama ya Jumuiya ya Ulaya nimetoa hukumu ya haki ya kutokumbukwa, inayotoa agizo la kufutwa kwa kumbukumbu ya zamani  inayoombewa kufanywa hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post