HAMISA ABWATUKA KISA MABUZI

MWANAMITINDO kiwango Bongo, Hamisa Hassan Mobeto amepangua tuhuma ambayo amekuwa akitupiwa na  watu wanaomuona aking’aa kisha kudai anatumia mgongo wa wanaume tofautitofauti (mabuzi).

 
Mwanamitindo kiwango Bongo, Hamisa Hassan Mobeto
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Hamisa alisema amekuwa akisikitishwa na tabia hiyo ya watu kumnanga kwenye mitandao ya kijamii kuwa anatupia picha nyingi ili kujiuza kwa mabuzi kitu ambacho si cha kweli.
“Kiukweli asiyekujua hakuthamini, nasema hivi kutokana na watu wengi wamekuwa wakinisema vibaya hasa katika mitandao ya kijamii, wanikome kwani kila mtu ana maisha yake na mimi sitegemei mabuzi kuishi mjini, nina mpenzi wangu mmoja tu,” alisema Mobeto

Post a Comment

Previous Post Next Post