Gazeti hili limebaini kuwa wengi wa wanaonunua
sabuni hizo, kama Dettol, Rungu, Family na Life Bouy, hawanunui kwa
ajili ya tiba badala yake hununua kulingana na zinavyonukia na
zinavyotoa taka mwilini.
Endrew Mlungu, mkazi wa Buguruni Dar es Salaam,
aliyekuwa akinunua sabuni hizo maeneo ya Buguruni Chama, alisema kuwa
anapenda kutumia Life Bouy kwa sababu akiogea zinamtakatisha na huziona
taka zikimtoka wakati anajisugua.
Anasema pale hali yake ya kifedha inapokuwa si
nzuri, hutumia sabuni nyingine lakini akiwa nazo anainunua kwa kuwa
humuacha mwepesi na akioga, hufanya kweli.
“Nikiogea sabuni tofauti na hii najisikia kama
sijaoga na hata nikiangalia sakafuni wakati najisugua sioni taka kwa
maana hiyo hazitoi na hazinisafishi vizuri,” anasema Mlungu.
Mlungu anafafanua kuwa hafahamu kama ni dawa, na
inawezekana kwa sababu ni dawa ndiyo maana akiogea inamtakasha, hivyo
hana haja ya kusubiri kuandikiwa na daktari kwa kuwa zinapatikana kwa
urahisi.
Sikujua Saidi mkazi wa Mbagala Dar es salaam,
anasema kuwa anapenda kutumia sabuni ya Rungu kwa kuwa inanukia vizuri
sio kama sabuni zinazopendwa kuwekwa kwenye gesti za uswahili ambazo
ukiogea kila mtu anakuhisi vibaya.
Anaeleza kuwa hata bei yake ni rahisi kwani akitoa Sh 1,000 anapata tatu, tofauti na sabuni nyingine huuzwa Sh 1500.
Richard Mwinyihija anasema kuwa hafahamu chochote
kuhusu sabuni zipi dawa na zipi za kawaida anachoangalia ni ipi anaipata
kwa ukaribu anapoihitaji.
Anafafanua kuwa anapohitaji sabuni huangalia bei
na ataipata wapi, kama anapita njiani na kukuitana na sabuni hana haja
ya kusubiri daktari amuandikie.
“Kama wao wangekuwa wanajua umuhimu wa sabuni hizi
kutolewa kwa maelekezo ya daktari zingeuzwa kwenye maduka ya dawa,
lakini zinauzwa huku kama zina madhara tutaumia wengi nani anajua kama
ni dawa mimi mwenyewe na kukaa kwangu Mjini sijui, naona nikinunua hizi
ndiyo kuelimika, ”anasema Mwinyihija.
Ustaadhi Salum anasema kuwa anashangaa kusikia
kuwa hizo ni sabuni dawa kwani amekuwa akinunua kila anapozihitaji na
mahali popote
- Mwananchi
Post a Comment