![two](http://i0.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/11/two.jpg?resize=461%2C288)
Mkurugenzi wa Idara ya Kinga kutoka taasisi ya Saratani Ocean road Julius Shija amesema kuwa takwimu zinaonyesha kuwepo kwa saratani ya mdomo na koo kwa kiasi kikubwa kuliko miaka iliyopita Tanzania.
Kwenye sentensi ya pili akasema >>> ‘Watanzania wasipende
kuiga mambo ambayo si sahihi bila kujua madhara yake kama kufanya
mapenzi kwa njia ya mdomo, saratani ya mdomo ipo na nyingine
zinasababishwa na zinaa’
Anasema kwenye kupokea wagonjwa wapya kila siku kwenye taasisi hiyo,
Wagonjwa waliopata saratani hiyo mdomoni na kwenye njia ya juu ya hewa
baada ya kujamiiana kwa njia ya mdomo wanaongezeka na sasa wanapokea
Wagonjwa 500 mpaka 600 tofauti na kipindi cha miaka ya tisini mwishoni na miaka ya elfu mbili mwanzoni walipokua wakipokea Wagonjwa 200-300.
![lovers 1](http://i0.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/11/lovers-1.jpg?resize=416%2C275)
‘Kufanya
mapenzi na kuhusisha mdomo kunaleta saratani kupitia mdomo na sehemu ya
juu ya hewa, virusi hivi vikifika kwenye sehemu ya juu ya hewa na
mdomoni na vikakuta kuna mchubuko au uwazi wowote vitaingia kwenye hizi
chembechembe za fizi kwenye ulimi na kwenye njia ya juu ya hewa,
vitapenya ndani na kuharibu zile chembechembe na zitaanza kukua na
kusababisha saratani’
Kwa kumalizia anasema virusi hivi kikawaida vinakuwa kwenye sehemu za
siri na vinasambaa kwa njia ya kujamiiana na vinasababisha baadhi ya
saratani kwenye sehemu za siri kwa mfano saratani ya shingo ya uzazi kwa
Wanawake
Post a Comment