
Na Karoli Vinsent
SIKU moja kupita baada ya Ripoti ya utafiti uliondaliwa na
taasisi ya isiyokuwa ya kiserikali ya TWAWEZA kumpa nafasi kubwa Waziri
mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya ufisadi wa Richmond, Edward Lowassa
kwamba ndiye anayefaa kumrithi Rais anayemaliza muda wake Jakaya Kikwete
kwenye uchaguzi mkuu mwakani 2015 na kuwapiku wanasiasa wengine ikiwemo
Waziri mkuu Mizengo Pinda na wengine ndani ya chama cha Mapinduzi CCM ,
Sasa Ripoti hiyo imeanza kupingwa na wadau mbalimbali ndani
ya chama cha mapinduzi CCM,na kusema ripoto hiyo imejaa ubabaishaji
mtupu wenye lengo wakuwadanganya watanzania kuwaamini kwamba viongozi
hao ndio wanafaa kumbe sio kweli.
Akipinga Ripoti hiyo ya TWAWEZA waziwazi, ni Naibu Waziri wa
Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Jannuary Makamba ambaye
amesema hata utafiti wenyewe umejikitia sehemu moja tu tena mjini na
haujafika hata katika visiwa na vya unguja na pemba na misingi hiyo
inazidi kushusha hazi utafiti wenyewe.
Makamba ambaye ni Miongoni mwa wasaka urais kutoka ndani ya
chama cha Mapinduzi ambaye amejiapiza kufa na kupona kushika nafasi
kumrithi Rais anayemaliza mda wake Jakaya Kikwete ameyasema hayo leo
Jijini Dar es Salaam alipokuwa anazungumza na Redio ya Magic Fm katika
kipindi cha Morning Magic,
Ambapo alizidi kwenda mbali zaidi huku akionekana akimbeza
Msaka Urais Mwenzake kutoka chama cha Mapinduzi CCM na mbunge wa monduri
Edward Lowassa,na kusema inasikitika kuona mtu zaidi ya miaka kumi
akiusaka urais na watanzania wanamjua leo nafasi yake imeshuka sana
kupitia utafiti huo,
Makamba ambaye Vilevile ni kiongozi kijana kutoka
ccm,aliendelea kusema CCM kinasifa 13 wakati wa kumteua mgombea wa urais
ambazo ziliwekwa tangu mwaka 1985 ambapo sifa zipo wazi ikiwemo sifa za
uadilifu,
Vilevile Makamba akatolea mfano 1995 ambapo wakati wa
wakumtafuta mgombea kupitia CCM, walitumia sifa hizo na wakati huo
walikuwepo wanasiasa maarufu,ila wakati wa kwenda Mkoani Dodoma na
Wagombe hao maarufu wakataliwa na CCM na akachaguliwa mgombea ambaye ni
ajulikani kabisa na akasema kuwa CCM haichagui kiongozi kutokana na
Umaharufu kama aliyokuwa nao Lowassa.
Kwa upande wake mwandishi wa Habari kutoka Redio Mario Joseph
mwalukusa alisema ripoti hiyo inamakosa mengi kwani imewaaangalia watu
wa mijini tu na kuwaacha watu wavijini na akaongeza kuwa ni wazi
kutakuwa na njama zinafanywa ili kumbeba mtu ambaye anarekodi za uchafu
ili achaguliwe na watanzania
Post a Comment