Wanafunzi,
leo naendelea na somo hili nililoanza wiki iliyopita.Kwenye elimu
hakuna ukomo, kumwita mtu aliyemaliza ngazi fulani ya elimu kuwa amefeli
ni kosa la kufikiri ambalo wazazi na wanafunzi wengi wamekuwa
wakilifanya. Kusema kweli fikra hizi zina madhara makubwa kisaikolojia,
hivyo ni muhimu zikaepukwa kwa vile baada ya kufeli kuna kufaulu,
kinachotakiwa ni kutafuta njia nyingine kwa kufuata muongozo ufuatao.
HATUA MPYA
Baada ya matokeo yasiyotarajiwa kutoka, mwanafunzi na wazazi wanatakiwa kuwa na mtazamo mpya kuhusu njia nyingine ya kufanya. Mtazamo huu hautakiwi kufanywa harakaharaka, kama baadhi ya wanafunzi walionipigia walivyotaka wazazi wao wawafanyie, yaani kumaliza na kutangaziwa papohapo nini kinafuata.
Inashauriwa kuwa baada ya kufeli, mwanafunzi anatakiwa kutuliza mawazo yake kwa siku zisizopungua 21, huku wazazi nao wakitumia muda huo kutafakari njia za kufanya bila kumvunja moyo mtoto wao hata kama uwezo wa kumuendeleza ni mdogo.
KUTOKUBALI MABADILIKO YA HARAKA
Jambo jingine la muhimu kwa wanafunzi waliofeli ni kutokubali kubadili tabia zao kwa kuiga haraka makundi ya vijana walioko mitaani. Mara nyingi mabadiliko hayo hutokana na matumizi mabaya ya muda unaokuwepo ambao awali wanafunzi husika walikuwa wanautumia kwa masomo.
Muda wa ziada unapotumika vibaya kwa kukaa vijiweni huweza kuathiri tabia na kupoteza mwelekeo wa kukabiliana na changamoto zinazokuwepo wakati huo za kutafuta shule na kusahihisha makosa.
Mara nyingi wanafunzi wanaomaliza hasa wa kike wanapokubali kuiga tabia za wenzao waliopo mitaani kwa kuungana nao katika matembezi na harakati za ujana huweza kuwasababishia mimba, magonjwa ya zinaa, kupoteza imani kwa walezi na wazazi hivyo kuweka mazingira magumu ya kusaidiwa. Hata wavulana nao hujikuta wanaingia kwenye makundi yasiyofaa.
KUFANYA UTAFITI
Mwanafunzi anapofeli na kurudi nyumbani na kukaa kwa kipindi alichoshauriwa anatakiwa aanze kufanya utafiti wa jinsi gani anaweza kujiendeleza kupitia kwa rafiki zake.
Hii itawasaidia wazazi ambao hawana mwamko wa elimu kupata njia sahihi za kumsaidia.

Post a Comment