Mama mzazi wa Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa ameitupia
lawama kamati ya Miss Tanzania kwa kushindwa kutimiza mahitaji ya mtoto
wake ili kumwezesha kwenda kushiriki mashindano ya Miss World.

Mshindi wa Miss Tanzania 2013 Happyness Watimanywa akiwa na Mama yake mzazi
Akizungumza na E-newz wa Eatv leo, Mama Happiness amesema amekuwa akifatilia kwa kamati hiyo lakini wamekuwa wakimzungusha.
“Wanasema hiki wanasema hiki, kwamfano kama introduction shooting
wakasema kwamba is very expensive,kwahiyo mimi nikajitolea nikalipa
milioni moja down payment, tangu mwezi wa tano nilikuwa nawaambia mpaka
two weeks ago hawana jibu lolote, mimi naogopa mwanangu asije akashushwa
kwenye stage, wewe huna visa hauruhusiwi kuja kushiriki shindano hili.
Haya hela ya shooping ambayo ni shilingi milioni tano walipaswa wamlipe
mtoto mpaka leo bado siku mbili mtoto anaondoka Jumamosi leo
wanamkabidhi tiketi bado hawajampa hela ya shooping sasa mtoto anaendaje
bila maandalizi, ndiyo maana nchi yetu kila mwaka inakuwa ya mwisho,”
alisema Mama Happiness
Post a Comment