Katibu wa Itikadi na Uenezi, Ndugu Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo ya makao makuu Lumumba, leo asubuhi. |
Ziara hii ya Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahaman Kinana ni muendelezo wa Ziara za Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi ambazo zimekuwa zikiendelea kote nchini tangu Sekretarieti hiyo ilipoteuliwa mwanzoni 2012.
Malengo ya ziara hii ni kukagua uimara wa Chama katika mikoa hiyo pamoja na kujenga na kuhimiza Uhai wa Chama katika kanda ya kusini ambayo kwa muda wote imeendelea kuwa ngome muhimu kwa Ushindi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Lakini pia ziara hii inalenga Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2010 - 2015 ambayo imeendelea kutekelezwa kwa mafanikio na Serikali katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Tunawaomba wananchi wa Mikoa ya Kusini kuwa tayari kujitokeza kwa wingi katika Mikutano ya hadhara iliyoandaliwa na kusema kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili ili ziweze kufanyiwa kazi na kutekelezwa mara moja.
UMOJA NI USHINDI.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Post a Comment