
Na Nova Kambota, Dar es salaam, Tanzania
Habari
kubwa hivi sasa barani Afrika ni mapinduzi ya umma yaliyofanyika
Burkinafaso, makala haya ni mtazamo wangu kuhusu kitakachojiri kusini
mwa jangwa la sahara kuelekea 2030, mtazamo huu umejikita katika
kutathimini matukio yanayoendelea kusini mwa jangwa la sahara na hali ya
kisiasa kwa ujumla, fuatana nami katika maandishi haya ya kusisimua;
Kusini mwa jangwa la Afrika si salama
Dalili
za wazi zinaonyesha kuwa nchi nyingi za kusini mwa jangwa la Sahara
zipo katika hali mbaya zaidi ya nchi za kiarabu zilizopinduliwa kama
Misri na Tunisia , halikadhalika kwenye mataifa hayo ya kusini mwa
jangwa la sahara kuna ukosefu mkubwa zaidi wa ajira hivyo kufanya idadi
kubwa ya vijana kuwa wazururaji kuliko Burkinafaso ambayo imepinduliwa
hivi karibuni. Sasa ikiwa hali iko hivi kwanini viongozi wa mataifa ya
kusini mwa jangwa la Sahara hawachukui tahadhari?
Kwanini wanazidi kujisahau?
Viongozi
wengi wa kusini mwa jangwa la sahara wanategemea kuudhibiti upinzani
kwa msaada wa vyombo vya dola mfano mzuri ni hujuma kubwa dhidi ya
viongozi wa upinzani kwenye baadhi ya mataifa yanayounda jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Tatizo
kubwa la marais hawa nikule kudhani kuwa vyombo vya dola vinaweza
kuudhibiti umma, wanapaswa kujifunza kwa makini maana halisi ya nguvu za
umma na athari zake kwa muktadha wa siasa za taifa lolote ulimwenguni,
yatosha kuzingatia kuwa umma haujawahi kushindwa.
Vyama
vingi tawala vitakataliwa Kutokana na kushindwa kutimiza wajibu wake
kwa wananchi vyama vingi tawala vitakataliwakatika mataifa ya kusini mwa
jangwa la Sahara.
Kuanzia
miaka ya 1990 vuguvugu la vyama vya upinzani limeweza kuving’oa vyama
tawala kadha wa kadha mifano ya UNIP Zambia, KANU Kenya na PDS Senegal
hapa pia usisahau kuangushwa kwa chama cha UMD cha Fredrick Chiluba huko
Zambia kilipopoteza kwa Michael Satta wa PF.
Angukohili
la vyama tawala halikwepeki hasa kwa kuzingatia udhaifu wa vyama hivyo
katika kushughulikia shida za wanyonge ikiwamo bei za mazao, ajira na
kupanda kwa gharama za maisha, utegemezi mkubwa wa nchi za kiafrika kwa
wawekezaji kutoka nje ,uwekezaji ambao umeshindwa kuondoa umasikini una
kila dalili mbaya kwa vyama vya ANC Afrika Kusini, FRELIMO Msumbiji na
CCM Tanzania, kuelekea 2030 vyma hivi vimezidi kupunguza idadi ya kura
huku upinzani ukizidi kushika kasi kwenye nchi zao.
Marais
ving’ang’anizi watang’olewa kabla ya 2030 Mwanahistoria Jovitus Mwijage
katika kitabu chake “Major Events in African History” akielezea
kushindwa kwa viongozi wengi waliotwaa madaraka kwa njia za mapinduzi
mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanzano mwa miaka ya 1990 , katika
ukurasa wa 308 anasema “Under the auspices of the constitutions made by
them (African dictators), the ballots could not change the existing
leadership; therefore, the barrel of the gun eventually became answer to
those political puzzles.
Even
the constitutions made after the coups could not attend to the
interests of the masses. The leaders of the coups made the
constitutions, which were to ensure that their evil interests were
fulfilled. Such constitutions appeared in Uganda, Sudan, Angola, Congo,
Zimbabwe, Gabon, Togo and Rwanda”.
Hali
hii ya viongozi kadhaa wa kiafrika ambao awali walionekana kuwa
wawakilishi wa kweli wa wananchi lakini polepole wakazivunja miguu
katika za nchi zao ili waendelee kutawala hivyo kugeuka ving’ang’anizini
sababu nyingine itakayopelekea mapinduzi kwa nchi hizo.
Iwe
ni mapinduzi ya umma ama vinginevyo lakini marais ng’ang’anizi kama
Yoweri Museveni wa Uganda na mwenzake Paul Kagame wa Rwanda wamekalia
kuti kavu kwani wananchi hawataki ufalme ama usultani bali wanataka
demokrasia inayozingatia ukomo wa madaraka. Ikiwa watawala wa mataifa
haya wataendelea kukaa madarakani basi joto kisiasa halitawaacha salama,
wimbi la mabadiliko litawafagia mmoja baada ya mwingine kuelekea 2030.
Nova
Kambota ni mchambuzi na mwandishi wa siasa, hii ni sehemu ya maoni yake
ya hivi karibuni kuhusu mapinduzi ya umma na mwelekeo wa siasa katika
mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara. Nova Kambota anapatikana jijini
Dar es salaam, simu +255712 544237, barua pepe; novakambota@gmail.com , Blog; http://novakambota.wordpress.com
Post a Comment