Ni single mpya na video mpya! Hilo ndio jibu la alilouliza Lady
Jaydee kwa mashabiki wake kwenye ukurasa wa Facebook; Are you ready for
something new?! How about November 28th?! Stay tuned.”
Picha na Osse Sinare
Akiongea na East Africa Radio hivi karibuni, Lady Jaydee aliutaja
wimbo mpya atakaoutoa mwishoni mwa mwezi huu. “Mwezi wa kumi na moja
mwishoni natoa nyimbo mpya pamoja na video. Wimbo unaitwa Forever
nimemshirikisha Dabo mdogo wangu, toka mimi kuzaliwa ananifuata yeye.
Yeah ni ngoma ya kwanza nilikuwa namuacha apevuke kwanza akue na
ajisimamie.”
Pia kwenye ukurasa wake wa Instagram alitease mashairi ya wimbo huo.
“Haya mapenzi kweli I just can’t explain eeeeh, Utanielewa vipi
iiih Moyo wangu wote uko kwako when ur not around Ur not here with me
Ooooh baby i can’t breathe Unapotoka tu, usipokuwepo tu moyo wangu
#Forever #JideFeatDabo#Comingsoon.”
Post a Comment