Mwanamke
mmoja nchini China ambaye ni mjamzito amehukumiwa kifungo cha maisha
huku mume wake akihukumiwa adhabu ya kifo baada ya kushirikiana kumbaka
na kisha kumuua msichana wa miaka17.
Mwanamke
huyo ambaye anajulikana kwa jina la Tan Beibei alifanya kitendo hicho
baada ya msichana huyo kumsaidia alipoanguka barabarani ambapo
alimpeleka hadi nyumbani kwake na badala ya kumshukuru waliamua
kumfanyia kitendo hicho cha akishirikiana na mumewe kisha kumuua na
kuamua kumzika.
Mahakama
ya Heillojiang ya nchini humo imesema kuwa imewafungulia mashtaka ya
kuua,kubaka pamoja na kushambulia baada ya mwanamke huyo kujifanya ni
mgonjwa na kushirikiana na mumewe kumfanyia binti huyo kitendo hicho cha
kudhalilisha kisa wivu kwa madai alikua akitembea na mumewe.
Mahakama
ya juu ilikataa kuwapunguzia adhabu wawili hao baada ya kukata rufaa
kwa madai kesi hiyo ni kubwa na haina dhamana yoyote.
Kwa
mujibu wa mashuhuda msichana huyo aliyejulikana kwa jina la Hu alikua
akipita barabarani ndipo mama huyo alipomwomba msaada wa kumpeleka
nyumbani kwake baada ya kuanguka na msichana huyo kutii lakini alipofika
alikutana na maswaiba hayo.
Inaelezwa
kuwa baada ya kufika mume wa mwanamke huyo alimpa msichana huyo maziwa
ya mtindi na baadaye kuanza kumfanya kitendo hicho lakini hata hivyo
hawakufanikiwa kwani binti huyo aliweza kuwazidi nguvu na walipoona
imeshindikana walichukua blanketi na kumziba nalo usoni hadi alipofariki
dunia na kuamua kumzika.
Katika
utetezi wa mwanamke huyo mahakamani hapo alisema aliamua kufanya
kitendo hicho kwa sababu binti huyo alikua akitembea na mume wake.
Historia
inaonyesha wawili hao walishawahi kuwa na kesi mbalimbali kiwemo ya
kutaka kumbaka rafiki wa mtoto wao wa kike ambaye alikua akisoma naye
darasa moja.
Post a Comment