Mastaa mbalimbali Bongo wamefungukia sakata linalowahusisha vigogo wanaodaiwa kujichotea mabilioni ya fedha kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow huku kila mmoja akiwa na maoni yake juu.
JB: Mimi nimeumizwa sana na hiki kitendo cha baadhi ya viongozi kufanya hivyo kwa nia ya kujinufaisha wao huku wakisahau kuwa wanawaumiza wananchi ambao ndiyo walipa kodi.
BABY MADAHA: Sijui sana mambo ya Tegeta Escrow lakini naumia sana kusikia bilioni zaidi ya 300 zimechotwa na wachache wakati sisi wananchi tunaishi kwenye mazingira magumu.
BANANA ZORRO: Inasikitsisha kuona nchi yetu ya Tanzania ambayo bado ni maskini watu wanaiba pesa nyingi kiasi hicho wakati kuna watu wanakamatwa kila siku kwa kosa la kutochangia mirandi ya shule.
ALI KIBA: Mimi bwana hapa naona Serikali inawalea sana hawa watu maana sisi kama wananchi ndiyo tunaoumia katika hili. Hatuwezi kuishi na viongozi wezi, nadhani sheria iwashughulikie wahusika bila kuwaonea haya.
JOHARI: Wale wanaohusika wachukuliwe hatua ili warudishe hizo fedha na ziweze kuwasaidia Watanzania kuliko kula watu wachache wenye tamaa za kijinga.
SHIJA: Hakuna haja ya kukaa na mtu anayeitia doa nchi yetu, kifupi waliochota fedha hizo wanatakiwa kufungwa jela ili iwe fundisho kwa wengine.
Post a Comment