MATAPELI WAMTUMIA DAVINA FACEBOOK

Stori: Imelda Mtema WALE matapeli wanaotumia jina la Tanzania Loans, ambao huwadanganya watu kuwa wanatoa mikopo isiyo na riba, wameingia kwenye akaunti ya msanii wa filamu, Halima Yahaya ‘Davina’ katika mtandao wa facebook na kuwataka watu kuchangamkia mikopo hiyo.
Msanii wa filamu, Halima Yahaya ‘Davina’.
“Unajua mpaka sasa watu hawanielewi kabisa mimi, wanajua ni kweli ndiye niliyeandika kitu hicho, si kweli kabisa maana hata ndugu na marafiki zangu wamenishangaa sana na wengine kuanza kunisema kwamba nimeanza mambo ya utapeli,” alisema Davina.
Kampuni hiyo ya kitapeli ya Tanzania Loans, huingia katika akaunti za watu kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, hasa mastaa na kujifanya kuwashawishi watu wajiunge katika mikopo hiyo, kitu ambacho siyo kweli. Wananchi wanaombwa kuwa makini na kamwe wasiamini, ni matapeli hao!

Post a Comment

Previous Post Next Post