Kocha Mkuu wa Yanga, Mbrazili, Marcio Maximo.KOCHA Mkuu wa Yanga, Mbrazili, Marcio Maximo, anatarajiwa kurejea nyumbani kwao, mara baada ya mechi ya leo dhidi ya Mgambo JKT ya mkoani Tanga.
Yanga inatarajiwa kuvaana na Mgambo katika mechi ya raundi ya saba ya
Ligi Kuu Bara itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.Timu hiyo, hadi hivi sasa imefanikiwa kuvuna pointi 10 pekee
ikicheza mechi sita ya ligi kuu kati ya hizo, imefanikiwa kushinda tatu,
ikifungwa mbili na ikitoa sare moja.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya kamati ya utendaji ya
timu hiyo, kocha huyo ataelekea kwao kwa ajili ya mapumziko ya wiki
moja wakati ligi kuu ikiwa imesimama na tayari uongozi umemruhusu.
Chanzo hicho kilisema, kocha huyo atarejea kwao baada ya kuuomba
uongozi wa timu hiyo kwenda kuisalimia familia yake aliyoachana nayo
miezi michache iliyopita kabla ya kutua nchini kuinoa Yanga akimrithi,
Hans van Der Pluijm.
Kiliongeza kuwa, kocha huyo ataongozana na msaidizi wake, Mbrazili,
Leonardo Neiva ambaye amepanga kwenda kuisalimia familia yake.“Mara
baada ya mechi ya kesho (leo) dhidi ya Mgambo, Maximo atarejea kwao
Brazili kwa ajili ya kwenda kuisalimia familia yake aliyoiacha muda
mrefu, tangu ametua nchini hakurejea nyumbani kwao.
“Uongozi umeruhusu kuondoka kwa kuwa baada ya mechi hiyo dhidi ya
Mgambo, ligi itasimama kwa muda wa wiki mbili ili kupisha maandalizi ya
Taifa Stars.“Wanaoondoka ni Maximo na Neiva, hao akina Jaja (Geilson
Santos) na Coutinho (Andrey) bado haijajulikana kama watabaki au
wataondoka,” kilisema chanzo hicho.
Post a Comment