Kaimu
mkuu wa mkoa wa Singida na mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahaya
Nawanda,akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya kunawa
mikono duniani, matumizi ya vyoo bora duniani na usafi wa mazingira kwa
mkoa wa Singida.Maadhimisho hayo yamefanyika katika kijiji cha Mgongo
kata Shelui wilaya ya Iramba.
Na Nathaniel Limu, Iramba
WANAFUNZI
wa kike ambao wamefikia umri wa kubalehe, kipindi cha hedhi hulazimika
kuacha masomo na kukaa nyumbani takribani siku 60 za masomo kwa mwaka;
imeelezwa
Imedaiwa hali hiyo kwa kiasi kikubwa, inachangiwa na ukosefu wa mazingira rafiki shuleni kwa wanafunzi wa kike waliobalehe.
Hayo
yamesemwa na mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone, wakati
akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya kunawa mikono
duniani, siku ya matumizi ya choo duniani na wiki ya usafi wa mazingira
kimkoa, yaliyofanyika katika kiiji cha Mgongo Wilayani Iramba.
Alisema
tafiti za kisayansi zinathibitisha kuwepo kwa uhusiano wa ongezeko la
mahdhurio ya wanafunzi shuleni linalochangiwa na uboreshaji wa
miundombinu ya maji na usafi wa mazingira, katika shule husika.
Kaimu
mkuu wa mkoa wa Singida na mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahaya
Nawanda,akimpongeza meneja wa shirika la SEMA, Ivo Manyanku (aliyekaa)
kwa kazi nzuri ya kuhamasisha wananchi wa wilaya ya Iramba kujenga vyoo
bora na kuvitumia.
“Katika
shule ambazo hazina miundo mbinu ya maji na usafi wa mazingira, hali
huwa mbaya mno kwa wanafunzi wa kike waliobalehe. Hali hii huwalazimu
kukaa nyumbani kipindi chote wanachokuwa katika hedhi, huku masomo
shuleni yakiwa yanaendelea”,alifafanua katika hotuba yake iliyosomwa kwa
niaba yake na mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahaya Nawanda.
Akisisistiza,
alisema kwa wastani kwenye shule zisizo na miundo mbinu rafiki kwa
wasichana kama maji safi, vyoo bora na vichomea ‘pad’, msichana husika
hupoteza takribani siku 60 za masomo kila mwaka.
“Hii
inamaana kuwa tunahitajika kuboresha hali ya usafi na mazingira pamoja
na miundombinu muhimu katika shule zote, ili matokeo makubwa sasa
yaweze kifikiwa katika sekta ya elimu”,alisisitiza zaidi.
Meneja
wa shirika la SEMA, Ivo Manyanku akizungumza kwenye kilele cha
maadhimisho ya siku ya kunawa mikono duniani, matumizi ya vyoo bora
duniani na usafi wa mazingira kwa mkoa wa Singida.Maadhimisho hayo
yamefanyika katika kijiji cha Mgongo kata Shelui wilaya ya Iramba.Kulia
ni kaimu mkuu wa mkoa wa Singida na mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahaya
Nawanda.
Katika
hatua nyingine,Dk. Kone ametoa wito kwa jamii kushirikiana na Serikali
kuhakikisha kila shule inakuwa na huduma ya vyoo bora pamoja na sehemu
maalumu za kunawa mikono, ili kuwakinga wanafunzi dhidi ya maradhi
yanayoenezwa kwa njia ya uchafu.
Mkuu
huyo wa mkoa alitumia fursa hiyo kuyashukuru mashirika ya siyo ya
kiserikali ya Water Aid Tanzania na SEMA kwa mchango wao wa hali na
mali ambao umefanikisha kwa kiwango cha juu maadhimisho ya mwaka huu.
Baadhi
ya wakazi wa kata ya Mgongo kata ya Shelui wilaya ya Iramba,
waliohudhuria kilele cha maadhimisho ya siku ya kunawa mikono
duniani,matumizi ya vyoo bora duniani na usafi wa mazingira kwa mkoa wa
Singida.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Post a Comment