MGANGA ANAYEDAI KUMNG’ARISHA MENINAH ATOBOA SIRI NZITO

Na Stori: Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani
Mganga aliyejita-mbulisha kwa jina moja la Kimweri ameibuka na madai mazito kuwa ndiye aliyemng’arisha staa wa kike wa Bongo Fleva, Meninah Abdukareem ‘Meninah La diva’ hivyo kutoa siri nzito ambayo wengi hawakuijua.Kwa mujibu wa chanzo makini, mganga huyo amekuwa akimfanyia ndumba msanii huyo ili arudiane na aliyekuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinum’.

Staa wa kike wa Bongo Fleva, Meninah Abdukareem ‘Meninah La diva’.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, mganga huyo amekuwa akidai kwamba, huwa msanii huyo anatinga nyumbani kwake maeneo ya Mwananyamala-Komakoma jijini Dar kisha kumlilia shida yake akimtaka afanye juu chini kuhakikisha anamrudisha Diamond mikononi mwake.
Baada ya kukisikia chanzo hicho, waandishi wetu walikwenda nyumbani kwa mganga huyo na walipomuuliza ishu hiyo alikiri Meninah kufika kwake ili kufanyiwa ndumba arudiane na Diamond.
 Meninah Abdukareem ‘Meninah La diva’ akipozi.
“Yule msanii anayeitwa Meninah ambaye habari zilivuma kuwa anatoka na Diamond na kukanusha, huwa anakuja hapa kufuata tiba na kikubwa anachokitaka anataka nimvute Diamond ili warudiane,” alisema.
Meninah alipoulizwa kuhusu madai hayo aliruka kimanga na kudai hakuwahi kuwa na uhusiano na Diamond na wala hamjui mganga huyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post