Ni wiki nyingine tunakutana tena
kupitia safu hii nikiamini umzima na unaendelea vyema na majukumu yako
ya kila siku kama kawaida. Mimi namshukuru Mungu kwa kunikutanisha nanyi
tena kupitia ukurasa huu ambao unagusa maisha yetu kwa kiasi kikubwa.
Mpenzi msomaji wangu, leo nazungumzia vijana ambao wanaendelea na matendo yasiyo na tija maishani huku hali zao kimaisha zikiwa duni kupita maelezo, muda nao ukizidi kuyoyoma.
Katika umri huu ambao kijana ana nguvu nyingi na uwezo mkubwa wa kufikiri na kuchanganua mambo, inakuwaje anakuwa limbukeni wa kutumia muda mwingi kuwa bize na mambo ambayo hayamsaidii kwa lolote?
Mathalani, unakutana na kijana ambaye kwa kumuangalia tu unabaini yuko duni kimaisha ila umri wake unamruhusu kufanya kazi kwa nguvu na kuyabadili kabisa maisha yake lakini eti yuko bize na mambo yasiyo ya msingi.
Starehe zimekuwa zikichukua nafasi kubwa kwenye maisha yake. Yaani licha ya ufukura alionao, kidogo anachokipata kinaishia kwenye pombe! Jina lake limetawala kwenye vitabu vingi vya wageni kwenye magesti! Hata siku moja mtu huyu hawezi kuwa na mwisho mzuri.
Atasifika kwa kuwa na utitiri wa mademu, atakuwa ni mtu wa kusaka heshima baa kwa kutoa ofa kwa marafiki huku akihisi hata kesho atazipata pesa kama alizopata leo kumbe anajidanganya.
Sina hakika kama wapo waliokuwa na maisha ya sampuli hiyo kisha wakaishi hadi wanazeeke wakiwa na furaha. Wengi wamekuwa na furaha ya muda mfupi na baadhi wamejikuta hata wakifupisha umri wao wa kuishi.
Hata hivyo, jambo moja la muhimu ni kwamba muda huwa refa mzuri wa mchezo na wakati wa majuto ukifika, muda wenyewe utakukumbusha jinsi ulivyoupoteza kwa mambo yasiyo na mantiki.
Nilishawahi kueleza huko nyuma kuwa, maisha ni safari ndefu sana yenye misukosuko, mabonde, miba, milima na miinuko ya kutisha! Inahitaji watu waliodhamiria tu kuyafikia mafanikio maishani, kwani njia ya kufika kwenye mafanikio, siku zote huwa siyo nzuri sana.
Pia tukumbuke kwamba, kila binadamu hapa chini ya jua, amepewa masaa 24 tu kwa siku! Hata hao unaowaona wana mafanikio makubwa maishani mwao, wanautumia muda huohuo, yaani siyo kwamba wao wana masaa 50 kwa siku wewe una masaa 24, la hasha!
Lakini bahati mbaya sana ni kuwa, pamoja na kupewa kiwango sawa cha muda, tunatofautiana jinsi ya kuutumia! Kuna ambao kupoteza dakika moja tu ni tatizo kwao lakini utashangaa wapo ambao siku nzima inapita wala hawajafanya lolote la msingi.
Swali kubwa kwako wewe kijana ni je, umejiandaaje na mwisho wa ujana wako pale nguvu ulizonazo zitakapofika mwisho? Uko tayari kukubaliana na ukweli halisi baada ya uwezo wako mkubwa wa kufikiri ulionao kufika mwisho?
Nikusihi tu kuachana na matumizi mabaya ya muda maishani mwako, ujana ulionao kwa sasa ipo siku utafika mwisho kama jinsi ambavyo kila jambo hufika mwisho. Usikubali kabisa hapo baadaye muda uanze kukukumbusha jinsi ulivyoupoteza, wakati huo ukiwa na hali mbaya ya maisha na tayari ujana ulishafika ukingoni!
Tumia muda mwingi kwa sasa ungali kijana na nguvu nyingi kwa mambo ya muhimu tu ili uwe na kesho isiyo na majuto.
Jitenge sana na starehe, chakarika kadiri uwezavyo, achana na maneno mengi na porojo zisizo na maana, fanya kazi kwa nguvu, kumbuka muda huwa haurudi nyuma!
Pombe, wingi wa wapenzi, starehe na anasa haviwezi kukusaidia chochote maishani mwako zaidi vinaweza kuwa ndiyo vizuizi vya kukukwamisha kuyapata mafanikio na kuwa na mwisho wenye kusikitisha.

Post a Comment