Mvulana mwenye umri wa miaka 12 auawa na polisi Cleveland, Marekani

Tamir E. Rice, akiwa katika bustani ya mjini Cleveland, Novemba 26 mwaka 2014. Picha za kamera zaonyesha  jinsi alivyokua akicheza na bastola yake bandia.
Tamir E. Rice, akiwa katika bustani ya mjini  Cleveland, Novemba 26 mwaka 2014.  Picha za kamera zaonyesha jinsi alivyokua  akicheza na bastola yake bandia. REUTERS/Cleveland Police
Na RFI

Mauaji ya mvulana mwenye umri wa miaka 15 katika mji wa Cleveland katika jimbo la Ohio, nchini Marekani yamezua hisia tofauti baada ya utata kuendelea kufuatia kifo cha Michael Brown, raia wa Marekani aliyeuawa na polisi mwezi Agosti mwaka 2014.

Mvulana huyo mwenye umri wa miaka 12 alikua akicheza na bastola feki, kabla ya kuuawa na askari polisi . Tukio hilo lilirekodiwa na kamera za polisi na kuwekwa hewani Jumatano Novemba 26.

Katika video, kijana huyo mdogo, Tamir Rice, anaonekana akicheza peke yake na bastola feki katika eneo la mjini karibu na maduka, huku akiinyoshea dhidi ya kila mpita njia anaye muona kama kujifurahisha.

Ghafla, gari la polisi likasimama kwenye nyasi mbele ya kijana huyo. Askari polisi mmoja akatoka ndani ya gari na kuanza kumfyatulia risasi.

Hakuna sauti inayosikika katika video hiyo, lakini kwa mujibu wa mkuu wa polisi, askari polisi hao walimuomba kijana huyo kuinua mikono. Hata hivo inaonekana kuwa askari polisi aliyehusika na kitendo hakua na uzoefu. Askari polisi huyo, mwenye umri wa miaka 26 alikua na miezi minane tu tangu alipoanza kuhudu katika polisi.

Hatua ya polisi iliyochukuliwa haraka ingeliweza kuepukwa kwa mujibu wa familia ya tamir Rice, ambayo iliomba video hiyo irushwe hewani.

Maafisa wawili wa polisi walisimamishwa kazi, huku wachunguzi wakisubiri ushuhuda wa wapita njia wanaoonekana katika video. Kama ilivyokua katika kesi ya Ferguson, jopu la wanasheria litaamua au la kufungua mashitaka.

Post a Comment

Previous Post Next Post