
Mkurugenzi wa taasisi
ya Mkubwa na Wanawe, Yamoto Band na Wanaume Family, Said Fella amesema
amejipanga kugombea ubunge wa jimbo Kigamboni, Dar es Salaam kwenye
uchaguzi mkuu mwakani.
Fella ameuambia
mtandao huu kuwa anachukua uamuzi huo ili kutetea watu wake katika eneo
lake ambao anaona wanakosa huduma kutokana viongozi kutosimama vizuri.
“Kama Mungu akinijalia uhai mrefu nina uhakika nitagombea katika jimbo
la kigamboni,” amesema Fella.”Ndipo ninapoishi mimi. Naomba Mungu iwe
2015, sitaki kuchelewa.”
Fella amesema kujiingiza kwake kwenye siasa hakutaathiri shughuli zake za kusimamia wasanii na tayari amejiandaa kwa hilo.
“Mimi naendesha
familia yangu nina maduka yangu na yanaenda vizuri, lakini bado nafanya
muziki na unaenda vizuri. Kwa sababu maduka yangu nimefungua kabla hata
muziki wa bongo fleva sijaujua na mpaka sasa hivi yapo. Wasanii wangu wa
TMK wapo.
na Bongo 5
Post a Comment