SIMBA
SC imetoa sare ya sita mfululizo tangu kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, baada ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar, Uwanja wa
Jamhuri, Morogoro jioni ya leo.
Ushindi huo, unawafanya Mtibwa wafikishe pointi 14 kileleni mwa ligi hiyo, wakati Simba SC imefikisha pointi 6 leo
Simba SC
ilikwenda kupumzika ikiwa tayari inaongoza kwa bao 1-0, lililotiwa
kimiani na beki wa kimataifa wa Uganda, Joseph Owino dakika ya 35 kwa
kichwa akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Emmanuel Okwi.
Hali hiyo
iliwafanya vinara wa hao wa Ligi Kuu wapate bao la kusawazisha dakika
ya 58, mfungaji Mussa Hassan Mgosi aliyetumia makosa ya beki wa kulia,
William Lucian ‘Gallas’ kuchanganyana na kipa wake, Manyika Jr.
Mtibwa Sugar: Said
Mohammed, Hassan Ramadhani, David Luhende, Andrew Vincent, Salim
Mbonde, Shaaban Nditi, Mussa Ngosi, Mohamed Ibrahim, Ame Ally, Mussa
Nampaka na Ally Shomary.
Simba SC: Peter
Manyika, William Lucian ‘Gallas’, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan
Isihaka, Joseph Owino, Jonas Mkude, Ramadhani Singano ‘Messi’, Awadh
Juma, Elias Maguri/Amisi Tambwe dk76, Said Ndemla na Emmanuel Okwi/Uhuru
Suleiman dk75.

Post a Comment