Mkurugenzi wa Idara ya Tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Dk. Margaret Mhando akifungua kongamano hilo la kisayansi.
Na Andrew Chale, Bagamoyo
SERIKALI
kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imepongeza juhudi za
makusudi zinazofanywa na Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) katika
kushughulikia masuala ya afya kwa jamii huku ikiahidi kushirkiana kwa
ukaribu.
Hayo
yalisemwa jana mjini hapa na mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Tiba wa
Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Dk. Margaret Mhando, aliyemwakilisha
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk.Donan Mmbando wakati wa ufunguzi wa
kongamano la 31 la Kisayansi na Mkutano mkuu wa mwaka wa TPHA
unaoendelea katika ukumbi wa Stella Maris, Bagamoyo.
Dk.Margaret
Mmbando alisema kuwa juhudi za dhati zinazofanywa na wadau wa afya
serikali inazitambua na watahakikisha wanaendelea kuungana nao kwa hali
na mali ilikuisaidia jamaii kwenye mambo yote ya msingi hususani masuala
ya afya.
"Tunaipongeza
TPHA kwa juhudi hizi za dhati kabisa katka ukuaji na ustawi wa sekta ya
afya. Hivyo pia naamini baada ya kongamano hili kwa muda wa siku tano
kila atakayetoka hapa atajifunza mambo makubwa na ya msingi katika
mustakaba wa sekta hii" alisema Dk.Margaret Mhando.
Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga (kulia) akimkaribisha, Dk. Margaret Mhando kwenye ufunguzi huo.
Aidha aliwataka TPHA kutanuka zaidi kuwa na matawi mengi ikiwemo kufika pembezoni mwa nchini ilikuweza kutanua huduma zao hizo.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa TPHA Taifa, Dk.Elihuruma Nangawe alisema
kongamano hilo la kisayansi la 31, linatarajia kuwa la siku tano na
kutarajia kumalizika Novemba 28 ambapo wataalamu wa afya na wadau
watajadilina mambo mbalimbali ya afya hapa nchini.
Naye
Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga alisema kongamano
hilo ni la kuwakutanisha wataalamu ili kubadilishana ujuzi, uzoefu na
kutoa mapendekezo namna ya kuleta mabadiliko katika jamii.
“Kongamano
la kisayansi na mkutano mkuu wa mwaka unahusisha wataalamu wa kisayansi
wa ndani na nje ya Tanzania ambapo watajadili masuala ya jamii na
maendeleo ya milenia,” alisema Dk. Kisanga na kubainisha kwamba shughuli
hiyo itahitimishwa Novemba 28.
Mkutano
huo leo unaingia siku ya pili ambapo wajumbe wa TPHA, wanachama na
wadau wa sekt za afya na mambo ya jamii wameendelea kujadili mambo
mbalimbali katika ukuaji wa sekta ya afya hapa nchini.
Mwenyekiti wa TPHA Taifa, Dk. Elihuruma Nangawe akitoa lecture katika kongamano hilo.
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo wakifuatlia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
Mgeni rasmi Dk. Margaret Mhando kwenye picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua kongamano hilo.
Post a Comment